Daniel Mjema na Rehema Matowo
TUKIO la kujeruhiwa vibaya Dk Stephen Ulimboka, jana kulilichochea hasira ya madaktari ambapo kundi la madaktari liliingia wodi hadi wodi katika hospitali ya rufaa ya KCMC na kuwatoa madaktari kazini.
Taarifa zilizopatikana hospitalini hapo zilisema, madaktari hao waliwatoa kwa nguvu wenzao waliokuwa wakiendelea kutoa huduma katika hospitali hiyo wakiwamo madaktari raia wa kigeni.“Ni balaa maana madaktari wameingia wodi moja hadi nyingine hadi wodi ya wazazi na kutushurutisha tusitishe kutoa huduma kama njia ya kupinga kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka”, alidai mmoja wao.

Madaktari hao walikuwa wakitembea na Laptop zikiwa na picha za Dk Ulimboka, akivuja damu huku wengine wakiwa na picha zilizochapishwa kwenye karatasi wakionyesha kila mtu wanayekutana naye.
Madaktari hao walikusanyika katika mgahawa uliopo jirani na chumba cha kuhifadhia huku wakipaza sauti wakitaka tukio la Dk Ulimboka liweke historia nchini katika kupigania haki za madaktari.
Huku wakikataa kupigwa picha wala kunukuliwa majina yao, madaktari hao wamesema watasitisha kutoa huduma zote zikiwamo za dharura kama Serikali haitatoa kauli ya kuridhisha juu ya tukio hilo.
“Pinda (Mizengo-Waziri Mkuu) si amesema liwalo na liwe basi na sisi tunasema haturudi kazini kwa sababu usalama wetu ni mdogo na sisi tunasema liwalo na liwe”walisikika madaktari hao wakisema.

Hata hivyo madaktari katika hospitali za serikali na vituo vya Afya katika wilaya za Same, Mwanga,Rombo, Hai na Moshi waliendelea kutoa huduma kama kawaida huku wakisita kutoa maoni yao juu ya tukio hilo.
Waandishi walipotembelea wodi mbalimbali na kuzungumza na wagonjwa, walisema wengi wao wameruhusiwa japo hawajapona na vitanda vingi hospitalini hapo vimebaki vitupu.
Mgomo katika hospitali hiyo ulianza Jumatatu wiki hii, ukihusisha madaktari walioko kwenye majaribio wapatao 80 lakini tukio la Dk Ulimboka limechochea hasira hadi za madaktari bingwa.
“Tunasubiri tamko la Serikali lakini isipofanya hivyo hata sisi hatuwezi kuingia kazini maana hili ni tukio la kinyama sana…hatuaamini kama ni Tanzania”, alisema mmoja wa madaktari bingwa.
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali mbalimbali kwenda KCMC, jana walijikuta wakirudishwa walikotoka kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea hospitalini hapo.
Mbali na kutopokelewa kwa wagonjwa wapya wanaohitaji kulazwa, lakini kliniki zote za wagonjwa wa kisukari, ukimwi na wale waliofanyiwa operesheni zimefungwa rasmi kutoa huduma kwa wagonjwa.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment