NI wiki nyingine tunakutana nikiamini kwamba umzima kabisa na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mimi namshukuru Mungu kwa kuendelea kuonesha upendo wake kwangu kwa kunipa uwezo wa kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, utakumbuka wiki iliyopita nilianza kuzungumzia sababu ambazo zinawafanya baadhi ya wasichana wenye umri mdogo kung’ang’ania mapenzi ya watu wazima ambao wanaweza kuwaita baba au babu zao.
Yaani imegeuka kuwa fasheni, mabinti wengi sasa wanadai vijana siku hizi hawana mapenzi ya kweli, wamekuwa walaghai kiasi kwamba wakiingia kwenye mapenzi nao ni sawa na kujiingiza kwenye matatizo.

Katika kuthibitisha hilo, baada ya kuandika makala haya nilipata ujumbe kutoka kwa dada mmoja ambaye aliandika hivi:
“Kaka Zekaima nakupongeza kwa makala yako, ni nzuri na umeandika ukweli mtupu. Mimi nina miaka 26, kwa muda mrefu nimekuwa nikiingia kwenye uhusiano na wanaume wenye umri unaoendana na mimi lakini nimekuwa sidumu.
“Nimekuwa ni mtu wa kuchezewa kisha kuachwa solemba kwa kipindi kirefu tangu nilipoingia kwenye ulimwengu wa mapenzi nikiwa na umri wa miaka 17.
“Baadaye nikabaini vijana hawana mapenzi ya kudumu, wamejaa usanii. Mwaka juzi nikapata mwanaume ambaye ana umri wa miaka 52. Yeye mke wake alifariki. Tulienda tukapima na kubaina tuko safi, akanioa.
“Huwezi kuamini mpaka leo hii nina mtoto mmoja sijawahi kujuta kuwa na mwanaume huyu. Ananipenda, ananijali na kunipatiliza katika kila ninalotaka.”
Kwa ujumbe huo unaweza kuona ni kwa jinsi gani sasa hivi wasichana wengi wanatamani kuwa na wapenzi watu wazima. Wiki iliyopita niliishia kuzungumzia sababu ya kwamba, watu wazima wamepevuka kiakili na kimwili. Sasa namalizia…
5. Wameshafanya makosa mengi, wamejifunza
Mtu mzima ni lazima atakuwa amepitia uhusiano na watu wengi. Atakuwa amepata uzoefu mkubwa kwani atakuwa amefanya makosa mengi na kupitia hayo atakuwa amejifunza, hawezi kuyarudia.
Kwa maana hiyo mwanaume mwenye umri umri mkubwa akiingia kwenye uhusiano na kabinti ni vigumu kukakwaza, kila atakalotaka kulifanya ambalo atahisi atamkosea ni rahisi kuliacha hivyo kumfanya msichana aliyeingia kwenye uhusiano naye kutopokea samahani za kila mara kwa mara.

6. Hawaigizi
Ni kweli wapo watu wazima wale tunaowaita mafataki ambao wanapomtokea binti mdogo lengo lao si kuoa bali ni kuonja penzi kisha huingia mitini.
Hata hivyo, uchunguzi unaonesha watu wazima wengi wanajua kupenda na wanaposema hivyo wanamaanisha kweli, hawaingizi sanaa na ndiyo maana ni wepesi wa kuhudumia, kubembeleza na kuchukua nafasi ya ‘ubaba’. Hicho kinawafanya wasichana wengi kukimbilia huko.

7. Hawana wivu wa kijinga
Wapo ambao wana wivu kweli lakini uchunguzi unaonesha kuwa, watu wazima wengi hasa wale walio kwenye uhusiano hawana wivu wa kijinga unaoweza kuwa kero.
Hawana tabia ya kupiga simu kila mara na kuuliza uko wapi, hawana maswali kama vile; ‘yule uliyekuwa unaongea naye ni nani’, kwa kifupi watu wazima wakipata kile wanachokitaka hawana ile kumfuatilia mtu licha ya kwamba wakibaini wanamegewa wanaumia sana na ni wepesi wa kuchukua maamuzi magumu.
Ni hayo tu kwa leo lakini siku zijazo tutaona madhara ya msichana kuingia kwenye uhusiano au kuolewa na mwanaume ambaye kiumri anaweza kuwa baba au babu yake. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine.

www.globalpublishers.info.
2 comments:
true. wanaume watu wazima hawana headaches kama masharobaro. any man under 40 years ni pressure tu maana no matter what u do u can never satisfy him.
kwa mnaopenda vi-rengeti boys take notes
Post a Comment