Rais Mstaafu wa awamu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Mchezaji bora wa mwaka kutoka timu ya Simba na Taifa Stars Shomari Kapombe tuzo yake ya mwanamichezo bora wa mwaka wa katika tuzo za zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Shomari Kapombe pia amezawadiwa kitita cha shilingi milioni 12 kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo kampuni ya bia ya Serengeti kutokana na ushindi huo wa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka
Shomari Kapombe mchezji bora wa mwaka akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa tuzo hizo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Simba huku akiwa ameshikilia tuzo yake na mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 12 za kitanzania kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Serengeti Richard Wells, kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda na wa pili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa iliyofanikiwa kushiriki mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 1980 mara baada ya kuwakabidhi tuzo ya heshima usiku wa kuamkia leo
Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na kutoa nasaha zake katika utozji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akitoa shukurani zake mara baada ya kukamilika kwa utoaji wa tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo.
Baba mwenye uzao wa mabondia Mzee Matumla kulia akikabidhi tuzo ya mwanamchezo bora wa kigeni katika soka Emmanuel Okwi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo,
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris katika hafla hiyo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Coast Union ya Tanga na Timu ya taifa Salim Amir akikabidhi tuzo kwa mchezaji Shomari Kapombe
Mpiga picha wa siku nyingi Athmani Hamisi akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa kiume katika mchezo wa VoliboMbwana Ally huku akisaidiwa na msaidizi wake
Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane akizungumza katika hafla ya utozi wa tuzo hizo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwanamichezo bora wa Tanzania.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Olimpiki Maalum Heri Suleiman
Mzee Ali Hassan Mwinyi akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane katikati ni mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto
Mkurugenzi wa Radio Times Rehuru Nyaulawa akimkabidhi tuzo yake mshindi wa tuzo ya mchezo wa Wavu wanawake Evodia Kazinja.
Mwenyekiti wa TASWA akimkabidhi tuzo yake mchezaji bora wa mchezo wa Netiboli Lilian Sylidion kutoka kutoka Shule ya Filbert Bayi.
Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka 2011 mzee Ali Hassan Mwinyi wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo usiku huu ambapo Fullshangwe inakuletea moja kwa moja matukio mbalimbali yanayojiri hapa Diamond Jubilee usiku wakati wa utoaji wa tuzo hizi, Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo Masoud Saanane, Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Mark Bomani
Wadau kutoka Serengeti wakiwa katika hafla hiyo ya utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells akijadili jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyoTeddy Mapunda katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Radio One na mtangazaji wa ITV Deo Rweyunga akiwa kazini pamoja na mtangazaji mwenzake Fatma Nyangasa katika hafla ya tuzo za mwanamichezo bora usiku huu.
Wadau mbalimbali na waandishi wa habari
Makamu Mwenyekiti wa Simba na Geofrey Nyange katikati akiwa katizo hafla hiyo kulia ni Jamal Rwambo mdau mkubwa wa michezo na kushoto ni Maulid Kitenge Makamu Mwenyekiti wa TASWA
Mdau Emmanuel na maiwaifiu wake kushoto pamoja na mdau wa masumbwi Zuena Kibena
No comments:
Post a Comment