ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 10, 2012

TIGU, A NETWORK OPPORTUNITIES CONFERENCE AT RENNAISANCE HOLLYWOOD HOTEL LA.

CEO wa TIGU Inc bwana Nduse Sebabili Akifungua mkutako kwa kumkaribisha Mgeni rasmi Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, nchini Marekani na Mexico, Mkutano huo ulijulikama kama Tanzania American Business Conference, Developing Business relationship" uliofanyika Rennaisance Hollywood Hotel, Los Angles, California. Mkutano huo ulifana na Watanzania wengi walijitokeza kuhudhuria na kupata fursa ya kutangaza kampuni zao. Mkutano huo ulihusisha Watanzania waishio Marekani na wale waishio Tanzania akiwemo mwanamitindo maarufu na bosi wa Mitindo House Khadija Mwanamboka, bwana Mbaruku Magawa ambaye ni Meneja Masoko na Huduma Jamii wa PPF,  Meneja Uhusiano wa PPF bi. Lulu Mangele, Meneja wa Sheria wa PPF bwana Nicander Kileo na bwana David Shambwe Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa NHC.
Kwa upande wa Marekani kulikuwa na makampuni na watu wengi waliojitokeza akiwemo Mshauri wa Biashara na mwandishi wa kitabu "The 7 powerful lessons to succeed in Business" ndugu Yassini A Kapuya na CEO wa ESM Travel ndugu Elias Mwita.

Mgeni rasmi Mh. Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akizungumza katika mkutano wa TIGU. Mh.Balozi aliwasifu Watanzania kwa umoja na juhudi wanazozifanya kimaendeleo na kuwaomba waendelee kwa ari na moyo wa namna hiyo.
 Mkurugenzi wa TIGU Inc akiongea machache.
Ndugu Lomba Mtango Mkurugenzi, wa TIGU Inc

Ndugu, Mbaruku Magawa ambaye ni Meneja Masoko na Huduma Jamii wa PPF, 
Ndugu Elias Mwita CEO wa ESM Travel akiongea katika mkutano huo

 Bwana David Shambwe Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa NHC.
Bi Khadija Mwanamboka Mwanamitindo na bosi wa Mitindo House akiongea machache siku hiyo ya mkutano.
 Bi Eliserena Kimalo, CEO wa Jambo Child Africa Hope, Akiongea machache mkutanoni hapo.
 Washiriki  wa mkutanoni huo wakimzikiliza Mh balozi Mwanaidi Sinare Maajar
 Meza ya mabosi wa PPF wakimsikiriza bosi wao Mbaruku  Magawa akiongea juu ya utendaji wa PPF.
Baadhi ya viongozi na waandaaji wa TIGU wakifuatilia mkutano
Wageni waliofika kwenye mkutano huo wakifuatilia jambo
 Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Bi Nancy mkurugenzi wa TIGU Inc, CEO Wa TIGU Inc, Nduse Sebadili, Mh Cyril S Ndaba, South Africa General in Los Angles, Ahmed Issa na Iddy Mtango
Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Marekani wakipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar.
Kwa picha zaidi Bofya Read More



 CEO wa ESM Travel Elias Mwita Ukodak Moment na washiriki pamoja na Mkurugenzi wa TIGU Iddy Mtango Mwisho.
 Bi Khadija Wa Mitindo House Ndani ya Nyumba...!
Wageni waliokuja maalum kwenye mkutano wa TIGU wakipata picha ya pamoja.
Walimbwende waliofika kwenye mkutano wa TIGU wakipata picha ya kumbukumbu.
Ny Ebra mwakilishi wa vijimambo New York akipata Ukodak moment na Afisa wa Ubalozi, Mindi Kusiga, kwenye Red Carpet,

Picha na EBRA NY


No comments: