ASEMA HATA WANAOTAKA KUUVUNJA WALETE MAONI YAO YATASIKILIZWA
Elias Msuya
MWENYEKITI wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao hata kama ni ya kutaka kuvunja Muungano katika mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya. Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho kuna vuguvugu la kutaka Zanzibar ijitenge, linalofanywa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIK), na kusababisha machafuko visiwano humo.

Jana, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari kutangaza kuanza rasmi kazi kwa tume hiyo tangu ilipozinduliwa rasmi April 13, mwaka huu, aliweka wazi msimamo huo unaoondoa mkanganyiko katika suala hilo. Kumekuwapo sintofahamu kuhusu msimamo wa Serikali juu ya Muungano, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza suala hilo kama moja ya tunu za Taifa, ambayo haitakiwi kujadiliwa kwa lengo la kuuvunja. Jaji Warioba alifafanua kwamba, tume hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwamba itakusanya maoni yote na kuyaratibu, ili kupata Katiba wanayoitaka wananchi wenyewe.
“Tume inafanya kazi kwa kufuata sheria. Na kwa kuwa klatika mchakato ni lazima tuanze na Katiba ya sasa, kwanza wananchi waseme upungufu wake. Wananchi wako huru kupendekeza, kwa mfano, kuwepo kwa Serikali yaani Bunge na Mahakama, labda wanataka tuwe na Rais dikteta, waseme,” alisema Jaji Warioba na kuongeza: “Kuhusu Muungano, tutayapokea maoni yote. Kama wanataka mambo ya Muungano yapunguzwe, au yaongezwe, Serikali moja au mbili au wanataka tuvunje Muungano, yote tutayapokea. Tusiseme watu wamezuiwa, hakuna aliyezuiwa.”
Akifafanua kifungu cha tisa cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayotumika katika mchakato huo, Jaji Warioba alisema Katiba haiwezi kuundwa kama hakuna nchi, ndiyo maana, suala la Muungano limewekwa kuwa la msingi. Kifungu hicho kinazungumzia mambo ya msingi (tunu za taifa), ambayo Tume ya Katiba itayazingatia wakati wa kukusanya maoni ya wananchi. “Muswada wa kwanza uliyataja hayo mambo ya msingi kama matakatifu, lakini marekebisho yaliyofuatia yalibadilisha na kuweka kuwa mambo ya msingi. Tume inayazingatia kwa sababu huwezi kuunda Katiba kama hakuna nchi.
Katiba tuliyonayo inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano,” alifafanua Jaji Warioba. Kuhusu tume hiyo kufanya kazi Zanzibar kabla Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi, Jaji Warioba alisema Katiba ya Zanzibar haisemi hivyo, badala yake inaelekeza kutoa taarifa tu. “Utaratibu uliopo ni sheria kuwekwa mezani, ndivyo ilivyo. Sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano zinatakiwa ziwekwe mezani, Baraza haliendi kujadili bali linapewa tu taarifa,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:, “Sheria hii ilitungwa Novemba mwaka jana na Baraza limekutana Januari mwaka huu.
Kwa utaratibu wa kawaida ilitakiwa iwekwe mezani kwenye Baraza mwezi huo, lakini kukawa na marekebisho mwezi Februari, baada ya hapo tukaipeleka. Sisi tume wala hatuna wasiwasi kwa sababu hilo limeshapita.” Kifungu cha 132 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinasema:
“Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kifungu cha 132 (2) kinasema, “ Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.”
Uratibu wa maoni
Kuhusu uratibu wa maoni ya Katiba, Jaji Warioba alitaja maeneo manne muhimu yaliyopewa uzito katika ukusanyaji wa maoni kuwa ni misingi ya Taifa ambayo ni uhuru, haki, udugu, amani, demokrasia na Serikali kutofungamana na dini yoyote, ingawa wananchi wake wana uhuru wa kuabudu, huku eneo la pili likiwa ni mamlaka ya wananchi.
“Kuna watu wanasema mamlaka ya wananchi hayakufafanuliwa kama vile Serikali, Bunge na Mahakama, tume ingependa kusikia maoni ya wakulima, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wanaume, wanawake, wazee, vijana na walemavu,” alisema. Aliyataja maeneo mengine kuwa ni malengo muhimu na msingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali, kama inavyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya tisa na eneo la Haki za Binadamu na wajibu wa jamii, kama inavyoelezwa katika sehemu ya tatu ya Katiba.
Marupurupu ya Tume/ Utaratibu
Akizungumzia madai kwamba wajumbe wa tume hiyo wanalipwa marupurupu mengi, Jaji Warioba japo hakufafanua mishahara ya wajumbe alisema hizo ni tetesi zisizo na ukweli.
“Nimesikia ‘speculations’ (tetesi) nyingi kuhusu hayo. Lakini, ninyi mtubane kwa kazi tuliyopewa ya kukusanya maoni….Hapa kuna wengine wana mapato ya chini kuliko huko walikokuwa, kwa kuwa tu wanaona umuhimu wa kulitumikia taifa lao… Sijui kila mtu analipwa kiasi gani…,” alisema Jaji Warioba. Akizungumzia utaratibu wa kazi wa tume hiyo, Jaji Warioba alisema kuwa tume hiyo itaanza kazi katika mikoa minane ya Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga.
Aliongeza kuwa tume hiyo itakuwa na nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, ikiwa ni pamoja nakala 500,000 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano, nakala 10,000 za Katiba ya Zanzibar na nakala 500,000 za Sheria ya Katiba ya mwaka 2012. Alisema baada ya kukusanya maoni hayo, Tume itakutana na mabaraza ya Katiba na mwishowe rasimu ya Katiba itafikishwa kwenye Bunge Maalum. Aliwataka waandishi wa habari kuwaelimisha wananchi ili waone umuhimu wa kushiriki katika mchakato huo.
Vurugu za JUMIK
Hivi karibuni visiwa vya Zanzibar na viunga vyake vilikumbwa na vurugu kubwa baada ya kundi la Uamsho kufanya vurugu na kutaka visiwa hivyo vijitenge kuwa dola huru. Hata hivyo, vurugu hizo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi, lakini juzi zililipuka upya na polisi kulazima tena kutumia nguvu kuzidhibiti.

Mwananchi
6 comments:
mzee mbunifu huyu mcheza maigizo hatutaki muungano hatuaki muungano hatutaki katiba mpya tumechoka viraka na kunyanyasha, hauna uhalali wowote mmungano leo hii imefanywa zanzibar mkoa na wakati ilikuwa nchi kamili,usawa hakuna so ndo maana hatutaki na hata hii katika mpya ikiwepo yatakuwa yale yale mtu huvaa viraaka lakini ikifika time viraka navyo huraruka so unahitaji nguo mpya na zanzibar yetu mpya isiyoungana na nyinyi
mdau washington d.c
Tupe mfano wowote wa nchi mbili au tatu zilizoungana na kila moja ika-maintain sovereign statehood yake. Maoni yako ni sawa na kutaka kuwa California au state nyingine yoyote ya USA iwe dola huru ndani ya United States of America.
mdau wa hapo juu(wa kwanza)kwani nani kawalazimisha kukaa bara?anzeni kurudi zanzibar huone kama utakatazwa!!tumewasitili sana nyinyi..rudini kwenu,kwanza nyinyi ndio mpo wengi bara kuliko waTanganyika waliopo Zanzibar..
Sumu ya ubaguzi isiwatinge msione mbele. Wote sisi ni ndugu, mbara, Mzanzibari pia ndugu zetu Wapemba!. Cha msingi ni kuondoa vikwazo vyote vinavyowakera wanachi wa pande zote mbili bila woga.
Wachangiaji (Anyn. 2 na 3),kama hamuezi kuchangia,basi ni bora mkakaa kimya. Kwani waZanzibari kuishi na kufanyakazi Tanganyika kuna tatizo gani??! Mbona kuna waTanzania wengi tu wako nje ya Tanzania,ilhali hakuna muungano wa aina yoyote. Pia kuna waChina kibao Tanzania,hususan Kariakoo DSM, hivi Tanzania iliwahi kuungana na China mwaka gani??!
Acheni kupotosha ukweli, hususan pale ambapo vitu vyote viko wazi kabisa. Mtu yeyote ambaye hajawahi hata kusoma makala inayohusu muungano, basi hatakuwa na hoja nzuri za kuhalalisha 'ukoloni' huu wa Tanganyika kwa Zanzibar. 'No research, no right to speak'!
Na kwa taarifa yako,usiifananishe Znz na California(Anyn.2), kwavile tangu hapo mwanzoni,haikuwahi kuwa 'sovereign state'. Znz ilikuwa ni nchi yenye mamlaka kamili tena iliyoendelea kiuchumi hata kuzidi nchi nyingi za Afrika,ikiwemo Tanganyika!Na pia ilikuwa ni mwanachama wa UN.
Kwaiyo tunapopigania haki zetu kama waZanzibari, basi hizo hoja zenu dhaifu ziwekeni pembeni. Tunataka muungano wa 'MKATABA' na sio wa 'KATIBA',ili kila nchi irudishe mamlaka yake kamili; Znz na Tanganyika. Ukoloni ukome tena!!!!
WELL DONE MDAU WA MWISHO WAPE WAPE VIJEMBE VYAO WAKITAKA KUCHEMSHA AU KUKOROGA WAKANYWA TOGHWA AU NGONGO SHAURI YAO
wanadhani bado tumelala na wanadhani hatujui historia yetu eti wametufadhili sana nani aliyekuja kutuomba kwa kutulaghai tuungane unajue hilo nani?
unajua kwamba baba yenu wa kanisa kwamba alituchukulia pesa zetu katika benki ya nje wakati baba yetu wa taifa alipo uwawa kwa njama kisa alishashtuka kwamba muungano huu Hautaki hauna manufaa kwa umma wa watu wa Zanzibar.Baba yenu wa kanisa alivyoona hawezi tena kumdhibiti baba yetu wa taifa alimuuwa na mwishowe kuchukua kiulani pesa za ummma wa watu wa zanzibar.
Na ndo maana leo hii DAR kumekucha na kunakucha kila leo(na wala hatuna wivu sisi tunachokitaka nchi yetu ya umma wa watu wa Zanzibar) wakati Zanzibar kumedorora na mnazidi kutowekea kiwingu cha kiza kila leo.Na njama zenu tumeshazingundua ndo maana hatutaki tena utumbo utumbo wenu HATUTAKI MUUNGANO HATUTAKI KATIBA MPYA YENYE VIRAKA VIRAKA TUNATAKA KATIBA MPYA NA ZANZIBAR YETU.
kuna mengi tu mkuu huyajui na sisi tunaijua historia yetu usithani ni wapuuzi kama mlivyo. so usilete hapa za kuleta ukajifanya NGUMIRIRE.
Na Dar-es-salaam ni mkoa wako? mali yako au umerithi kutoka kwa wazazi wako? au baba yenu wa kanisa kakurisisha?, tuabiye tujua kama umerisi tutatoka huko na kukuachia mkoa wako because itakuwa ni mali yako.
sijapata katika maisha yangu yote niliyoishi kuona mtu kama wewe aise!! mwisho kabisa wewe naona bora uende tena shule ukasome tena na ujifunze pia ustaarabu nakuona kama mtu wa sayari inginewe eti tutoke DAR, tutatoka usijali tupeni nchi yetu hatutaki muungano na wewe urudi kwenu kijijini because Iam very sure wewe si mtoto wa Dar hujazaliwa pale Dar wakuja tu ndo maana ustaarabu hunao.
mmetuchukulia mali zetu na kutufanya muflis ndo maana tuko huko kwenu kuja kuchukua nasisi chetu upo bwana mdogo/Bibiye.
na leo hii eti mnajidai kidomo domo mmetusitiri, nani kamsitiri mwenziwe? fanya reseach bwana mdogo/bibiye ujue historia na ujijua wewe vizuri ulivyo. na kwanza jina la DAR ES SALAAM Litolewe liwe MZIZIMA SI TUMEKUPENI Nyinyi hilo jina eti MZIZIMA unamzizimisha nani,na Tanganyika, Tanga-Nyika , hebu chunguza hayo majina mliyokuwa nayo zamani,Utumbo mtupuu.
sipo haba kuharibu hali ya hewa au kulumbana lumbana bila ya hoja.Naona si kosa lako hujui historia yetu ndo maana una kurupuka na kuja katika blog hii kuleta utumbo utumbo wako.
Hujui historia yenu wala ya kwetu.Ungeijua historia yetu ungenyamaza kimya ungeona aibu na fedhehaa kusema mmetusitiri na eti Zanzibar ni Sovereign state kama California. HAMNAZO Na ni akili za kijuha. Na ni aibu na fedheha ya hali ya juu mtu kama wewe kuchangia mada bila ya hoja na kuja hapa kuleta UTUBO UTUBO Wako.UJINGA WENU PELEKENI KWENGINEKO
DJ Luke Mkuu Niwekee Hii Cpmment Yangu PLEASE Wangu Na naomba sana Nisamehe Kama nimeharibu hali ya hewa katika blog yako.
Sema watu wakileta Kidomo domo na kujifanya too much to know bila ya kutoa hoja na kutokujua Historia ya yetu basi hawawezi kuachiwa lazsima watajibiwa kwa kiwembe kila kila walichokuja nacho hapa kutaka kuwanyoa wenzao na wao watanyolewa na hicho hicho kiwembe chao.NA Wanune na wapasuke na wale sumu tuwaonee.
HATUTAKI MUUNGANO, HATUTAKI MUUNGANO, HATUTAKI KATIBA MPYA NENDENI NA VIRAKA VYENU KAUNGANISHENI NA NCHI NYINGINEWE HATUTAKI MUUNGANO
NA INSHALLAH RAHMAN ATATUSAIDIA ATATUTOA KATIKA SHIMO LA GIZA LA MUUNGANO HUU INSHALLAH. AMIN.
MASALLAM
WASHINGTON D.C
Post a Comment