Advertisements

Tuesday, July 31, 2012

Gangamala, usiuze mechi, ni kosa kusema umechoka faragha!-3


UTAPOTEZA MVUTO WAKO
Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii inamaana ya kuongeza mvuto!
Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia.

Anakuomba leo, unamjibu umechoka, kesho tena unaweka ngumu! Hasara kwako hapo ni kupoteza mvuto wa kimapenzi, kwa maana atakapohisi kuhitaji tendo, kila akikufikiria, ataona wewe ni mtata na hueleweki, kwamba akikuomba utamtolea nje.
Kwa mwanamke ni hatari zaidi, kwani kwa wanaume wasio na uvumilivu, mwisho huishia kubakwa. Hata hivyo, mara nyingi hiyo haiishii hapo, tatizo hukua zaidi na zaidi kulingana na jinsi mgogoro wa kuwekeana ‘kauzibe’ unavyoshamiri ndani ya nyumba.
Ukiweza kumudu kumfurahisha mwenzi wako, anachokihitaji ukimpa kwa wakati. Maana yake atazidi kukuona lulu. Kila akiwa na wewe atajiona yupo huru kuomba huduma wakati wowote. Na pale utakaposema umechoka, itakuwa rahisi kukuelewa na kukuvumilia, kwani siyo kawaida yako.
KUSALITIWA NI NJENJE
Unambania kila siku, aendelee kukusubiri kwa kitu gani hasa? Kama ni mwanaume, maua yapo mengi ‘kitaani’, kwahiyo ataangalia kwingine kwa lengo la kutuliza mizuka yake. Ni vema ukitambua ya kwamba huyo siyo amoeba! Ni mtu hai anayehitaji huduma.
Kisaikolojia, ni mwanaume mmoja kwa mia, anayeweza kuvumilia kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi. Asili ya maumbo yao, hasa walio na afya timamu, hisia zao zipo karibu, kwa maana hiyo anaweza kuhitaji hata kila siku. Kama ni mwanamke, ni busara kulitambua hili.
Mwanamke anaweza kukaa muda mrefu bila kutamani tendo, lakini hatari kubwa ni kwamba uwezo wake wa kuvumilia ni mdogo mno pale anapokuwa jirani na mwanaume. Akiwa peke yake ni sawa, ila akiwekwa jirani na watu wa jinsia ya pili, mambo huenda kinyume chake.
Unafika nyumbani unalala mzungu wa nne, lakini kuna wakati ukigeuka na kumgusa, unamfanya ahisi kutaka huduma. Wewe unambania, hapo utamsababishia akiamka, afikirie mahali ambapo anaweza kupata tiba! Kwa muuza bucha, genge au hata houseboy!
Akiitwa barabarani atakuwa mwepesi kusikiliza kwa sababu mwili wake ni mzito na unahitaji kupunguzwa. Akiulizwa kama ana mume, atajibu hana na akisema anaye ataeleza kwamba hana noma! Akiombwa namba atatoa, mwisho wa siku, haki yako atapewa mwingine.
Usifikirie maumivu ya kusalitiwa, tafakari kuhusu jinsi unavyodhalilishwa. Kama binadamu na uhusiano wa kimapenzi, heshima ya kweli ni pale ambapo mwenzi wako anakutunzia ‘tamu’ yako kwenye mazingira yoyote yale. Akiitoa, ni sawa na kuvuliwa nguo! Pale unapopumzika na wengine hutulia hapohapo!
Hii inamaana kuwa hutakiwi kujiuguza uvivu katika suala la mapenzi. Toa huduma inayotakiwa, ikibidi ongeza vionjo kadiri unavyoweza. Kosa kubwa kwa wengi ni kwamba hawachukulii tendo kama ni jukumu la kutekeleza. Yaani ni wajibu! Wanaona ni kitu rahisi ndiyo maana kila siku wanalia.

www.globalpublishers.info

1 comment:

mjukuu said...

Neno hiloooo lipo mwake