ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 18, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA YA AJALI YA MELI ZANZIBAR


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
-Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Bandari mjini Zanzibar kuona ndugu zao waliookolewa wakiwa hai na waliofariki katika ajali hiyo[PICHA ZOTE NA
RAMADHAN OTHMAN IKULU]

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar.
Abiria waliyookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR
Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wa pili kulia) akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali alipofika
katika Ofisi za Shirika la Bandari, Malindi Unguja kupata taarifa
sahihi ya ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Sky Get ikitokea Dar es
Salaam kuelekea Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,IKulu.]

No comments: