Sasa wanaunda tume ya kuchunguza ajali, Tume ilitakiwa kuundwa kabla meli haijanunuliwa iliiwezeshe kujua ubora wa meli kabla haijaingia Tanzania lakini kuunda tume sasa hakuta saidia kurudisha maisha ya Watanzania wasiokua hatia yaliyokatizwa ghafla na uzembe na uroho wa kujipatia pesa za haraka haraka kwa kununua meli zilizopitwa na wakati na zisizolingana na hali halisi ya mazingira yetu huku wakijua fika uwezo wa meli ni kubeba watu 250 pia Meli hizo zilishasimamishwa kufanya kazi ya kuchukua abiria Washington State, Nchini Marekani lakini tamaa ya kujali matumbo yao bila kuthamini uhai wa Watanzania ndio maana hamuoni aibu kudanganya Watanzania kwamba uwezo wa Meli ni kubeba watu 300 na tani 26 za mizigo wakati mkijua kabisa uwezo wa meli ni watu wangapi.
Watanzania inabidi tuamke usafiri wowote unapokua umejaa kamwe tusikubali aongezeke abiria mwingine kwani kufanya hivyo ni kucheza na uhai wako pamoja na huyo abiria anayeongezwa halafu mwisho inapotokea ajali unaambiwa ni kazi ya Mungu kwanini tunakwepa majukumu yetu kwa kumsingizia Mungu? kwani Mungu ndie aliyekutuma kununua vyombo vibovu? kwani Mungu ndie aliyekutuma kuongeza abiria wakati ukijua uwezo wa meli inabeba abiria wangapi? Acheni hizo inabidi tubadilike sasa, unda tume kabla Meli haijanunuliwa au chombo chochote kitakachonunuliwa kusafirisha Watanzania.
Napenda kumpa pongezi kwa Waziri wa miuondo mbinu Mhe. Hamad Masoud Hamad kwa kukubali kujiuzulu na jua sio peke yake wapo watu chini yake mpaka yule aliyetoa majina ya abiria waliondoka kwa kudanganya Meli iliondoka na Abiria pamoja na wafanyakazi 248, bila kufanya hivyo hatutajifunza na maisha ya Watanzania yatapotea kila siku mpaka watalii watakimbia kwa usalama wa maisha yao hasa wanapokua Tanzania..
Ni Mimi Mkereketwa naependa Nchi Yangu na Watanzania wote ni Ndugu Zangu.
2 comments:
Kweli kabisa Tanzania imejaa uozo kwa ajili ya tamaa ya wachache.Nakubaliana kabisa na makala hiyo. Tena viongozi wetu ambao wengine walihusika katika kupitisha uingizwaji wa meli hiyo mbovu wanajidai nao wana simanzi kubwa. Nilipata kuongea na ndugu yangu huko bongo akaniambia eti hali ya hewa ilikuwa mbaya ndicho chanzo cha ajali. Kwa nini nahodha atie nanga bila kujua hali ya hewa ikoje huko endako? Pia wengine wanasema sababu meli ilijaza sana! Kwa nini nahodha atie nanga wakati meli imejaza zaidi ya uzito inayotakiwa kubeba!!!!!!? Kwa nchi yetu iliyojaa rushwa hata tukiweka wakaguzi wa kukagua meli kabla hazijatia nanga wakaguzi hao watataka rushwa ili mradi meli itazidisha uzito au kuruhusu meli mbovu itie nanga bila kujali maisha ya raia wetu. Kwa kweli inasikitisha sana tukizingatia ni juzi juzi tu hapa meli nyingine ilizama na kuchukua maisha ya wenzetu wengi.
At least watu wameanza kujiuzulu(take resposibility and be accountable).
Nimependa point ya kusema ni makosa matukioo mabaya yanapotokea kusema ni "kazi ya Mungu". Tuna utamaduni mbaya(haya nchi za nje hili lipo)wa kujidanganya kuwa ni "mapenzi ya Mungu" matukio mabaya na vifo vinapotokea. Sio mapenzi ya Mungu mtu afe, Mungu alipotuumba alitaka tuishi "eternally". Kifo ni kazi ya SHETANI aliyeleta dhambi, siyo Mungu. The Good News Of The Kingdom of God is, God is going to restore his original purpose. The bible says, "...there will be more death,....!"
Post a Comment