Tunapenda kuleta shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika kuuguza na kasha kusafirisha mwili wa ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa nyumbani Tanzania kwa mazishi.
Mwili ulisafiri salama na mazishi yalifanyika Jumanne ya tarehe 3 mwezi huu na mkewe kurejea hapa Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita
Shukrani za pekee kwa Madaktari na wauguzi wa Hospitali za Chuo Kikuu cha Howard na Chuo Kikuu cha George Washington, Viongozi wa Dini waliomhudumia katika siku zake za mwisho, kwa Kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries na washarika wake kwa kufanikisha ibada ya kumuaga ndugu yetu mpendwa, kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mbali na karibu ambao walijitokeza kumhudumia alipokuwa amelazwa na hata kusaidia familia kwa ushauri, hali na mali katika wakati mgumu waliokuwa wakipitia.
Tunaamini kuwa UPENDO mliouonyesha kwetu utaendelea kwa wengine kwani katika nyakati kama hizi, ni UPENDO pekee ulio nguzo kuu kwetu.
Mungu awabariki katika kila jema mfanyalo.
Asanteni
Kamati ya msiba
No comments:
Post a Comment