Katibu Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Bw.Omar Abdallah kushoto akipokea Mashine ya kupumlia wagonjwa(Oxygen Conamtrator) kwa niaba ya Hospitali ya Mwembeladu kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Said Amour,katikati Meneja wa banki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia,Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia,akimkabidhi Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar Bi.Zawadi Suleiman Msaada wa Vyandarua pamoja na mashuka 50 na vifaa mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Afisa Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Martha Edward akimpatia zawadi ya Tende Bi.Amina Ahamed alielazwa katika Wodi ya Wazazi kwenye Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki ya KCB kufika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa kwenye picha ya pamoja na wauguzi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki hiyo kufika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.
---
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wodi ya akina mama wajawazito katika hospitali ya Mwembeladu visiwani Zanzibar, ikiwa ni jitahada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina mama na watoto
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni nne na laki sita (4,600,000) vilikabidhiwa jana kwa hospitali hiyo na meneja wa tawi la KCB stone town Rajabu Ramia katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Ramia alisema msaada huo ulilenga kuepusha vifo vinavyoweza kutokea kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo na kuongeza kuwa huo ulikuwa ni muendelezo misaada mbali mbali ambayo Benki hiyo imekuwa ikitoa kwa jamii
Vifaa vilivyo kabidhiwa ni pamoja na mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumua (Neuro Oxygen Concentrator), shuka za kujifunika 50 na vyandarua 50.
Meneja huyo wa tawi aliongeza kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa afya ya mama na mtoto katika ustawi wa taifa na ndiyo maana imeona umuhimu wa kutoa ikipau mbele katika msaada huo kwa kundi hilo
Akipokea msaada huo, katibu wa hospitali hiyo Docta Omari Abdala aliishukuru Benki ya KCB na kusema kuwa msaada huo umekuja katika muda muafaka na kuongeza kuwa hospitali hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa vifaa jambo ambalo linawafanya wakinana mama kuikimbia.
“Hospitali hii ya Mwembeladu ni hospitali kongwe kuliko zote katika masuala ya uzazi hapa Zanzibar. Kwa kipindi kirefu, imekuwa kimbilio la wakina mama wengi wajawazito lakini kutokana na ukososefu wa vifaa, wakina mama wamekuwa wakiikimbia na kwenda hospitali ya Mnazi mmoja. Tunaishukuru KCB kwa kutusaidia vifaa hivi kwani vitasaidia kuboresha hali,” alisema
Katibu huyo alisema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza msongamano katika hospitali ya Mnazi mmoja ambayo akina mama wengi wakekuwa wakikimbilia
“Tunaomba mashirika mengine ya kiserekali na yasiyo ya kiserikali kuiga mafano wa Benki ya KCB kwa kusaidia sekta hii muhimu ya afya. Suala la afya linamgusa kila mwanadamu na kwa hiyo ni vyema tukashirikiana na serikali kuboresha huduma kwa kuchangia kama ilivyofanya KCB Bank,” alieleza.
CHANZO: GPL
Angalio, hicho kifaa kinaitwa oxygen concentrator na sio Oxygen conamtrator.
ReplyDelete