Friday, August 10, 2012

FAHAMU NAFASI YA UONGO KATIKA MAPENZI - 3


NINA Imani Mtakuwa Wazima Wa Afya Njema Na Mpo Tayari Kupokea Kitu Kipya Kutoka Katika Ukurasa Huu. Kwa Upande Wangu Nipo Sawa Kabisa. Siri Ya Kutokuwa Mtumwa Wa Mapenzi Ni Kujifunza. Jenga Tabia Ya Kujifunza Kila Siku Ili Uweze Kukomaza Uwezo Wako Katika Sayari Ya Mapenzi.

Marafiki Zangu, Msingi Hasa Wa Mada Hii Si Kuwafundisha Watu Wawe Waongo Au Kutetea Uongo Unakubalika Katika Mapenzi, La Hasha! Ninachojaribu Kueleza Katika Mada Hii Ni Kwamba, Kuna Wakati Ukweli Wako Unaweza Kuharibu Uhusiano Wako Na Mwenzako.
Hapa Katika Let’s Talk About Love Ninakuonyesha Baadhi Ya Maeneo Ambayo Yanakubalika Kudanganya (Kwenye Uhusiano) Ili Kujenga Uhusiano Ulio Imara. Sasa Twende Tukamalizie.

Ulikuwa Wapi?
Inawezekana Upo Kwenye Ndoa Na Kwa Bahati Mbaya Jioni Wakati Wa Kurudi Nyumbani Ulipitia Kwenye Mambo Yako (Siyo Usaliti Lakini) Na Pengine Hutaki Mkeo Afahamu Kwa Sababu Zako Binafsi.
Ili Kukwepa ‘Usumbufu’ Wake, Ukaamua Kuzima Simu Na Kuendelea Na Ratiba Zako Hadi UlipokUwa Sawa Na Kuanza Safari Ya Kurudi Nyumbani. Mkeo Kwa Wasiwasi Anakuuliza Maswali Huku Akitaka Kujua Ni Kwa Nini Ulizima Simu Na Mahali Ulipokuwa.
Kwa Kuwa Hukuwa Sehemu Mbaya Na Hutaki Ajue, Uongo Wa Kumwambia Kwamba Ulikuwa Kwenye Kikao Unakubalika Katika Eneo Hili.
“Samahani Mpenzi Wangu, Niliingia Kwenye Kikao, Kilikuwa Cha Ghafla. Bosi Alituita Bodi Nzima, Nisingeweza Kuingia Na Simu Ikiwa On, Lakini Unisamehe Mama, Nilisahau Kukujulisha Kutokana Na Presha Ya Kikao Chenyewe, Maana Kwa Sehemu Kubwa KIlihusu Idara Yangu,” Uongo Huu Utainusuru Ndoa Yako Huku Ukiendelea Kuwa Mwaminifu Kwa Mwenzako.

Vipi Kuhusu Kusifia?
Wakati Mwingine Ili Kumfanya Mpenzi Wako Ajisikie Kamili Unatakiwa Kumsifia Sana. Kikubwa Ni Kwamba Kutoka Ndani Ya Moyo Wako Unampenda Kwa Mapenzi Yako Yote, Msifie Kadiri Uwezavyo Ikiwezekana Sifa Ambazo Hana.
Utakuwa Unamdanganya Kwamba Yeye Ni Mzuri Zaidi Ya Miss Tanzania, Lakini Ukijua Kwamba Umeridhika Naye. Hakuna Sababu Ya Kumuacha Akiwa Na Mawazo, Akijifananisha Na Watu Wengine MAarufu, Akijihisi Kwamba Pengine Hakufai.
Mpe Moyo, Mwambie Boyfriend Wako, Anakuvutia Kuliko Ray Na Hemedi. Unajua Akianza Kujiamini Yeye Ni Bora Zaidi Ya Mastaa Wanaozimikiwa Na Wadada Wengi, Atakuwa Huru Zaidi Kwako.
Jamaa Anaweza Kuwa Wa Kawaida Tu, Lakini Ni Wako Na Upo Tayari Kuwa Naye Kwa Hali Yoyote, Kwa Nini Usimsifie Ili Muendelee Kudumu? Bila Shaka Umepata Kitu Kipya! Uongo Wakati Mwingine Unaokoa Penzi.
Hadi Wiki Ijayo Kwa Mada Nyingine, Usikose!
Joseph Shaluwa Ni Mshauri Wa Mambo Ya Mapenzi Anayeandikia Magazeti Ya Global Publishers, Ameandika Vitabu Vya True Love, Let’s Talk About Love Na Who Is Your Valentine Vilivyopo Mitaani.

1 comment:

  1. haja kaa fresh hii mkuu unawafundisha wanaume watudanganye siyo japo kuwa umeandika siyo niya yako lakini nilivyoisoma habari mpaka mwisho nimehishi ndo hivyo jamani huoni hata haya, nikweli niayako ilikuwa njema naliku uandishi kidogo umekutupa.

    kwa nini umdanganye mtu kwa nini, kumsifia ni vizuri sana lakini kama unajua kwamba hafanani mkeo na wema sepetu kwa nini umwambiye ni mzuri kama au kumzidi wema sepeu KWA NINI USIMWAMBIYE MAMA MIMI NAKUPENDA SANA TENA SANA HAKUNA MWANAMKE MNAYENIZINGUA/AU ATAKAYE NIZINGUA KWA MAISHA YANGU ZAIDI YAKO, NAKUPENDA KWA TABIA YAKO,KWA UCHESHI WAKO,UAMINIFU WAKO, UKARIMU WAKO,USOMI WAKO,UNAVYONIJALI MUMEO NA WATOTO ETC ukimsifia hivyo na kama anazo sifa hizo basi nitosha kabisa kumchanganya mama kama ana kupenda na wewe kikweli kweli

    cha pili kwa nini usimwambiye simu imeisha chargi au niliamua tu kuzima simu sijisikia leo kuzunguma na simu na mama aminiya kwamba mimi nakupenda wewe na sitofanya chochote kulisaliti penzi langu na mungu wangu ni shahidi maana yeye ndo anijuaye na anionaye kila vitendo vyangu ninapokuwa nje ya upeo wa mboni zako na yeye ndo atakaye nihukumu nikienda kinyume na penzi letu na atakaye kuja kunifichua na kunifedhehesha siku nikikusaliti niamini mpenzi kwa kauli zangu hizi kama unampenda kwali mkeo utakuwa unayasema haya

    siyo eti leo unazima simu halafu unamtafutia uongo jua kwamba uongo huzaa uongo na mwishowe utakuwa kila leo una jaribu ku cover uongo wako mwisho utaubukwa tuuu

    hakuna siri duniani au kumzingua mwenzio ukawa kila leo unaula na kujifanya mjanja mjanja kuna siku utaubuka tuu

    so mheshimiwa usiandike kuwafundisha wanaume maneno ya kutudanganya because jua kwamba hata na sisi wanawake tunayajua haya tena tuko expert ile mbaya tupe ukweli turidhike siyo longa longa za kitoto kila mtu mtu mzima kaingia kwenye uhusiano wa mapenzi kwa ridhaa yake siiyo kudanganywa danganywa kama toto bwegee

    haya ndo yangu ya leo

    mdau NY

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake