Kuna habari zinasambaa kwenye mitandao kwamba Chadema wanafungua tawi Uingereza. Hili si jambo baya lakini mkutano huu umeshitua watu wengi sana. Mkutano huu umeandaliwa kihuni na hii inaanza kutupa hofu wananchi kuhusu uwezo wa Chadema kuongoza nchi. Inasemekana ufunguzi huo utafanyikia kwenye baa tena usiku saa mbili. Ndugu Godbless Lema ndiye mgeni rasmi. Walioandaa mkutano huu hapa Uingereza inasemekana ni wajanja nawengine wanajihusisha na biashara haramu. Kama kweli Chadema iko serious kwa nini mkutano usiandaliwe sehemu ya kiheshima, ukafanyika mchana wakati kila mtu anaweza kufika, yakatolewa matangazo na watu wakaalikwa? Hata hivyo pamoja na watu wengi kutokukubaliana, utashangaa kuona mkutano huu unafanyika na kwenye mablog keshokutwa tutaona picha na hata kutangaziwa viongozi wa Chadema London...what a joke. Kama hali yenyewe ndiyo hii, all the best Chadema.
Asante.
Wako Hamis
Mtoa mada hoja zako hazina msingi. Nafikiri wewe ndiyo unaleta hoja za kihuni. Kama wewe ni muungwana ungetoa ushahidi wa tuhuma unazowazushia wenzako, ungeandika jina lako kamili, anuani yako, namba ya simu, na hata email yako. Kushindwa kutoa ushahidi wa tuhuma zako pamoja na identity yako, umetuthibitishi wasomaji kuwa inawezekana wewe si muungwana na unachuki binafsi na waandaji wa mkutano huo. Watanzania tupendane hata kama tuna itikadi tofauti za siasa. Unapowashutumu wenzako kuwa wanaandaa mkutano kihuni unapata faida gani? Je ni mikutano mingapi ya vyama vya siasa imefanyika usiku bar tangu tupate uhuru lakini hujalalamika?
ReplyDeleteChadema sidhani kama wako tayari kuongoza nchi may be in 10 years or so. wapunguze kwanza ukorofi, siyo lazima kutumia lugha za ugomvi
ReplyDeleteKwani wakifanya usiku kuna shida gani? Huku Ulaya hakuna shida hata kama umefanyika mkutano bar, kwani lazima watu wanywe? Acheni siasa za majitaka, wewe mmbeya uliotoa hoja hapo juu una uhakika gani kama CDM haiwezi kuongoza? Toa pointi za maana, achana na pointi za mitaani.
ReplyDeleteKati ya CCM na Chadema nanj mkorofi na Mgomvi?????? Nani anaetishia watu na mtemi??????? Mpaka kuzuia mikutano ya Chadema isifanyike???????? Nani mbabe???????? Chama gani visadi?????? Nani kasababisha nchi iwe na deni kubwa bila mafanikio??????? Hospital hazina hata incubator wala exray nani mkorofi na mgomvi kwa wananchi?????????. Hapo nimekupa list ndogo tu ili ufunguke akili, any way Ngoja nikusaidie jibu CCM ndo wagomvi na wakorofi je upo???????? Acha kuropoka tu Kama umehongwa sinia ya wali, au kofia na khanga za CCM. Chadema iko busy kuokowa nchi kwa kuwasuta na kuwapa facts CCM lakini narrow minded and brainwashed ppl wanasema sijui wakorofi Mala chadomo mala blah blah blah!
ReplyDeleteNchi imeshachukuliwa na Chadema ngoja utakapo patwa butwaa 2015. And that is in 2 yrs not 10 boo boo.
DJ Luke I took my time to write this pls weka comment yangu thank you.
ATL
Nadhani kama Chadema wanataka watanzania wawaamini ni muhimu wakaacha mambo haya . Hata mimi nashangaa kusikia kikao kinafanyikia baa.
ReplyDeleteHahaa mdau wa kwanza kaniacha hoi. Anamshutumu mtoa mada hajatoa identity wakati na yeye ni anonymous...bongo tambarare.
ReplyDeleteWewe unayesema ni sawa kufanyia vikao vya muhimu baa kwa sababu vimekuwa vikifanyika tangu tupate uhuru fikiria kabla hujalaumu wengine. Your argument ni kwamba "mbona CCM imefanya vikao baa lakini nchi ina maendeleo?". This is nonesense, Chadema wamekuja kama alternative to CCM sasa kama wanafanya yale yale kuna haja gani ya kubadilisha? Si bora tubaki na CCM!!!!
ReplyDeleteMdau wa kwanza kabisa nakubaliana na wewe,hivi we Mdau Hamis ebu acha kutupa habari za kubabaisha,kumbuka kwamba hii ni blog ya jamii na inasomwa na watu wenye akili zao ,sasa unavyotuambia eti kuna habari zinasambaa ,watu tunashindwa kukuelewa,yaani tungekuona wa maana sana kama ungetudhibitishia kwa vielelezo ,na sio kutupa habari za kubabaisha,nakushangaa sana ndugu yangu ,yaani karne ya sasa unaweza ukatoa hoja yako kwa kadamnasi bila kuwa na visibitisho,nafkiri watu watakuona kama ni mwendawazimu tu,kwa kusema kuna habari zinasambaa.je anayezisambaza ni nani?kama sio wewe.mdau hamis sijui rika lako.Ebu ndugu yangu jaribu siku nyingine kufikiria kabla haujakurupuka kuleta malalamiko yako katika jamii,Tambua hii blog haisomwi na wahuni,
ReplyDeletepili mdau hamis nakushauri kama umekosa cha kuandika ni bora ukawa unasoma comment za watu wengine itakuwa haijakupunguzia kitu.
tatu bila kukusahau Dj naomba uweke hii comment.
Asanteni kwa kuniazima masikio yenu.
Mdau.
wana DMV kazi kweli tunayo ivi kwenye jamii yetu ya sasa kuna mtu anaweza kuji-adress hivyo kwa umati,Ebu angalieni nature yenyewe ya ujumbe nanukuu (Kuna habari zinasambaa.....)kwa jinsi ujumbe wako ulivyo inaonekana haukuwepo kwenye tukio bali ulisikia,tungekuona wa maana kama ungetumbia ulikuwepo kwenye kikako cha izo,wana blog bado hatuwezi kukuelewa mpaka japo utakapo tuwekea hata kielelezo kimoja au japo uthibitisho.hayo mambo ya kusema eti kuna habari....blablaaa izo zilishapitwa na wakati wana DMV tunaitaji vielelezo,then ndo tunaweza tukafungua mjadara.
ReplyDeleteMdau Black Mpingo.
Nadhani Watanzania tuna safari ndefu, anasema amesikia na hakuwepo na hajui kiluzungumzwa nini na pia hajui kwamba watu walikunywa wakalewa wakashindwa kutoa hoja za mkutano. kama hivyo havikutokea shida ya nini? hata kama wangefanyia juu ya mti ni sawa tu kikubwa ni ujumbe umefika. sisi Watanzania tunamatatizo sio kwenye uongozi tu hata huelewaji. DJ luke ahsante kwa bunge lako huru siku njema
ReplyDeleteKikao kinafanyika bar sababu hatuna pesa za ufisadi Kama CCM. Chadema tunatumia jasho letu kuokowa nchi so bar hamna kiingilio itatusaidia sana kubaa matumizi kwani sisi hatuwezi kuibia walipa kodi ili tulipie hall tukanufaisha chama je nimekujibu vizuri mdau wa hapo juu uliecoment after comment nzuri ya ATL.?
ReplyDeletenawashangaa sana maana huyo mdau hakusema yeye ni mfuasi wa chama gani, lakini mnaisakama CCM kupita maelezo,
ReplyDelete