Nancy Baraza
Jopo maalum la majaji
lililoteuliwa na rais Mwai Kibaki kuchunguza tuhuma zilizokuwa
zinamkabili Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza kumdhalilisha mlinzi
mmoja katika duka moja kubwa mjini Nairobi, imependekeza, jaji huyo
kuondolewa madarakani.
Akisoma hukumu hiyo mjini Nairobi leo,
mwenyekiti wa jopo hilo, Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Augustino
Ramadhan, amesema Nancy Baraza akiwa mtumishi wa chombo cha kusimamia
sheria na haki hakutakiwa kwa namna yoyote kutenda kosa hilo dhidi ya
mlalamikaji Bi Rebecca Kerubo.Amesema kitendo alichofanya Nancy Baraza na ni cha utomvu mkubwa wa nidhamu na hivyo kupendekeza kwa Rais Mwai Kibaki kumwondoa katika wadhifa wake wa naibu jaji mkuu.
Nancy Baraza alituhumiwa kumnyanyasa na kumpiga Bi Kerubo tarehe 31 Desemba 2011, baada ya kutakiwa kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuingia katika duka hilo, utaratibu ambao umekuwa ukitekelezwa kwa wateja wote.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake