Mtoto aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu,Kadogoo
Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro akiwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian akiwa anahudumiwa na
manesi hospitalini hapo juzi jijini ArushA
Wafanyakazi wa Hopsitali ya Seliani wakiwa wanamuhamisha mtoto huyo kwenda Agha Khan baada ya kukosa kifaa cha kumpima
JESHI la Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada
ya Askari wake wa tatu kutuhumiwa kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16
wa jamii ya kifugaji anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa
Orkesmet Wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu.
Tukio hilo
lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012 majira ya saa tano na nusu katika
eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa jina
moja tu la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu kuiba
mbuzi wa jirani yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa eneo
hilo la Orkesmet.
Mashuhuda wanadai kuwa polisi hao baada ya
kumkamata mtoto huyo, walianza kumuadhibu bila huruma hali iliyopelekea
mtoto huyo kulazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika
Hospitali ya Selian iliyopo jijini Arusha.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa kutokana na kisa
hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa walitaka kufungua
mashtaka dhidi ya askari waliofanya unyama huo lakini walikataliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ndani
ya Hospitali ya Selian mama mzazi wa kijana huyo, Bi. Paulina Kalanga
alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani
na kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshumbulia kwa kumpiga bila kumpa
nafasi ya kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na haja ndogo
mfululizo na kisha kupoteza fahamu.
“Yaani walimkamata kijana
wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke ….. wakazishika
sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako cha silaha ya moto
ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza fahamu”alisema huku
machozi yakimtiririka
Taarifa zinasema kuwa polisi hao baada ya
kuona hali ya mtoto huyo imekuwa mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza
haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa ajili ya matibabu kabla ya
wanandugu kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance) kumkimbiza
katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.
Kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio
hilo alikiri kupata taarifa zake huku akisema kwa kifupi kwamba tayari
ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi
wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.
“Nimeshatoa
maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti
kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio
hilo”alisema
Hatahivyo,aliongeza kwa kusema kwamba endapo kuna
askari atabainika kuhusika na tukio hilo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake.
“Ikibainika askari amehusika basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa na hapa tayari uchuinguzi unaendelea”alisema
No comments:
Post a Comment