Thursday, August 30, 2012

HUYU NDO MAMA ALIYETAKA KUTUPA WATOTO WAKE MAPACHA KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA

Mama Theresia ni moja kati ya kina mama ambao ugumu wa maisha ulipelekea mpka kufikiria kwenda kuwatekeleza watoto wake mapacha.

Mama huyo ambaye ni mkazi wa Mbezi Darajani amesema mbali na hao mapacha ana mtoto mwingine wa kwanza anayeitwa Theresia mwenye umri wa miaka 3.Alisema kuwa baba wa watoto hao mapacha wa kiume Frank na Fred amekimbia na pia naye kipato chake ni kidogo na ameathirwa na ulevi kwahiyo hata kidogo anachokipata anashindwa kuwalea watoto wake

Mama Theresia mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa kwa sasa anahitahi mtu wa kumsaidia kupata pesa za kulipa kodi angalau ya miezi 3 ambayo ni shilingi elfu 45, na pia pesa ya mtaji wa biashara ya kuuza mboga au nyanya au Samaki biashara ambayo awali alikuwa akiifanya.

1 comment:

Anonymous said...

tutampaje msaada?