ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 30, 2012

SAFARI MARATHON KUFANYIKA SEPTEMBER TISA WAMAREKANI NAO KUSHIRIKI

 Mwenyekiti wa mbio za Safari Marathon Chris Honest akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na mbio hizo wa pili ni katibu wa mbio hizo Victor Molel
 
Tamasha la mchezo wa riadha lijulikanalo kama safari marathoni linatarajiwa kufanyika september tisa mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu za sheikh Amri Abeid jijini hapa.Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mwenyekiti wa mbio hizo Chris Honest alisema kuwa mashindano hayo kwa mwaka huu yameboreshwa zaidi na yanatarajiwa kufanyika jumapili ya septembrer tisa mwaka huu.Alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha wanariadha wakubwa wananchi wa kawaida na watoto kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya ,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Ethiopia na kwa mwaka huu wamepata nchi nyingine ambazo zimejiandikisha kushiriki ambazo ni South Afrika pamoja na marekani.Alisema kuwa mpaka sasa hivi watu zaidi ya 1000 wamejiandikisha kushiriki mbio hizo kwa kupitia njia ya mitandao ambapo alisema kuwa kwa wakazi wa mkoni hapa na jirani ambao hawajajiandikisha kushiriki kwa njia ya mtandao wanaalikwa kujiandikisha kuanzia september nne katika uwanja wa sheikh amri abeid huku akisema kuanzia siku hiyo namba za ukimbiaji pia zitaanza kutolewaKwa upande wake katibu wa mbio hizi za safari marathoni Victor Molel alisema kuwa kwa mwaka huu wameboresha zaidi mashindano kwani hata zawadi zimeboresha huku akibainisha kuwa kwa upande wawakimbiaji w akilometa 21 kwa wanaume na wanawake mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shilingi 1,000000 huku mshindi wa pili akipata kitita cha shilingi 6000000 na mshindi wa tatu akiondoka na kitita cha shilingi laki tatu.Kwa upande wa kilometa 10 ambao kilometa hizi zinawahusisha wanariadha walemavu mshindi wakwnza atapata kiasi cha shilingi laki mbili,wapili laki na nusu na watatu laki moja na huku akibainisha kilometa tano ambazo zinawajumuhisha watu wote watoto wababa,wamama na vijana mshindi wa kwanza atapata laki tatu wapili lakimbili na watatu atapata laki moja.,Alisema kuwa kwa mwaka huu pia wameboresha njia ambazo zitatumika na kutakuwa na usalama wa kutosha huku akitoa wito kwa wanchi mbalimbali wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano haya ya safari marathoni kwani mashindano haya yanasaidi kukutanisha na watu mbalimbali kutoka nchi mbalimbali na kubadilishana nao mawazo"sasa kwa mwaka huu barabara zitakazo tumika ni pmoj na mwenye round about-polisi station-NCAA round about,Goliondoi road-sokoine road-clock tower-boma road-municipal building- Ncaa roundabout-AICC -Sanawari-Kaloleni Road-Florida Roundabaut na kumalizia stadium road kisha kuingia uwanjani"alisema MolelAlisema kuwa siku hiyo pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwa pamoja na michezo ya watoto ,pmoja na bendi mbalimbali ambazo zitatumbuiza

No comments: