ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 4, 2012

Muungano waibua mpasuko CCM Zanzibar



Wanasiasa wawili wakongwe visiwani Zanzibar wanatoafautiana kimtazamo katika muundo wa Muungano uliyoyaunganisha mataifa huru mawili ya Tanganyika na Zanzibar Januari 12, mwaka 1964 imefahamika.

Wakiongea kwa nyakati tofauti toka vyanzo mbalimbali vya maoni yao, wanasiasa hao ni Hassan Nassor Moyo na Ali Ameir Mohamed ambao waliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Matamshi ya Moyo na Ameir yanajitokeza wakati huu huku kukiwa na vuguvugu kubwa la ajenda ya utoaji na ukusanyaji wa maoni ya wananchi ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania ulioibuliwa na Seriikali ya awamu ya nne Tanzania chini ya Rais Jakaya Kikwete.



Wakati Mzee Moyo akitaka uwepo Muungano mpya wa mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar, Ameir alisema nje ya muundo wa Serikali mbili kuna mwelekeo unaogofya wa kuyasaliti Mapinduzi ya 1964 ili kuviza historia ya chama cha ukombozi cha Afro Shiraz Party.

Ameir aliyewahi pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alieleza kuwa dhana ya Muungano na Mapinduzi ni kama watoto waliozaliwa wakiwa wameungana viungo vyao hivyo ni vigumu kuwatenganisha ghafla.

"Ukiwatenganisha bila ya utaalam watoto hao, maumbile ya maisha yao yanaweza kuleta hatari zaidi, uzoefu wangu kidogo unanionyesha hilo jambo mazingira yake ni magumu kutimia," alisema Ameir.

Ameir alisisitiza haja ya msingi kwa mataifa hayo kubaki na muundo wa sasa wa kikatiba ili kulinda misingi ya umoja, udugu na utengamano aliyodai ulianza tokea miaka 48 iliyopita.

Ameir alisema nje ya Muungano kuna mkakati utakaotoa mwanya kwa maadui wa ndani na walioko nje ili kuhatarisha umoja wa kitaifa na kuleta mgawanyiko utakaovitikisa visiwa vaya Unguja na Pemba.

Moyo kwa upande wake anapingana na mtazamo huo akisema haja ya kuendelea na Muungano wa kikatiba imepitwa na wakati huku akitaka wanachama wenye fikra mbadala ndani ya CCM wapewe nafasi ya kusilizwa bila ya kutishwa.
CHANZO: NIPASHE

2 comments:

Anonymous said...

namunga mkono hassan nassor moyo ukisoma historia yake utaona ni yeye kweli mwana muungano mzazi wake mmoja ametoka ruvuma na wapili zanzibar so yeye ni mtoto wa muungano daimu lakini fikra zake zimeona mbali ndomaana akona muungano huu hatufai na ni kweli apewe nafasi ya kusikilizwa bila kutishwa.

Anonymous said...

huyu dingi ameir ananiacha hoi eti watoto kuwatenganisha bila utaalam ni hatari kupigwa mabomu watu na kupoteza uhai wao anaona ni sawa bado tu tushikilie muungano utafikir kudra kutoka kwa rahman