Mwalimu Daniel Urioh. |
Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.
Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria.
Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.
Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?
Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.
Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na wanafunzi.
Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri.
Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.
Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya.
Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania.
Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.
Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.
Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737
Chanzo: www.kajunason.blogspot.com
9 comments:
Hivi watanzania tutakuwa na uelewa lini? Kama ni sheria kutokuzungumza kiswahili shuleni inapaswa mwalimu afuate. Hii ni free market economy, mwajiri yeyote anaye haki ya ku-terminate ajira wakati wowote anapoona inafaa. Sasa wewe umekatazwa kuongea kiswahili halafu unaongea hapo umekwenda kinyume na taratibu na mwajiri wako hivyo anayo haki ya kukufukuza kwa sababu umekiuka sheria, Hivi mpaka lini mtashindwa kuelewa, naona bado wengi wetu wana mawazo ya ujamaa na hicho ndicho kinachoturudisha nyuma. Hatujazoea kufanya kazi kwenye sekta binafsi tupo tupo tunafikiria kila mahali ni serikalini.....serikali yenyewe hii dhaifu ndiyo maana kila mtu anafanya analotaka. Samahani bw. Urio umekosea na unapaswa kufuata sheria ya mwajiri wako, na kama unaona huwezi si lazima uwepo hapo, mwajiri hawezi kufuata matakwa yako, wewe ndiyo unayetakiwa kufuata anachokuagiza la sivyo mlango upo wazi, kumbuka hiyo ni sekta binafsi ukitaka kuongea kiswahili unaweza kwenda mtaani. Discipline ya kazi ni kitu cha kwanza, shirika au kampuni haiwezi kuendelea kama watu kama wewe wanavunja sheria ( they don't comply). Tuna safari ndefu.
Wewe una shida una mambo yale ya ujamaa, eti kiswahili kimeleta amani? Kwani kujua au kujifunza english kunaondoa amani? Kwani wakati unajiunga na shule hiyo hukujua mission na objectives za shule? Kwa nini ulikubali kuajiriwa kama hukubaliani na lugha wanayofundisha? Hiyo ni sekta binafsi tafadhali uondoe mawazo ya ujamaa na kujitegemea, naona kama umebaki nyuma. Timiza masharti ya mwajiri wako kama huwezi ondoka, acha majungu ambayo hayatakusaidia, ongea english kama ulivyotakiwa, huwezi? ondoka.
Pole sana pole sana japo kuwa hasaidi ndugu yangu Daniel urioh, na wadau walio weka comment zao wanajifanya kujua kumbe majuhaa.
Niambiyeni wapi kizungu kimeleta amani?niambiyeni wapi wazungu wana imani na kutupenda sisi ngozi nyeusi kihaki na kikweli kweli, bila ya kututumia kwa manufaa yao?
mlioyoyasema wadau wenzangu hapo juu kidogo tu nakubaliana na nyinyi kwamba
Mwalimu Daniel Urioh afuate sheria za kazi ni kweli lakini amewekewa wazi na hadharani kuhusu hizo sheria za kazi? je shule hii wao wanafuata sheria za nchi walio wekeza? je wao wanafuata kanuni za kazi?
subutu mtu binafsi afunguwe shule marekani,bara la ulaya yeyote(European countries)uchina na ujapan asifuate sheria za nchi utajua kwa nini bawala haitwi swala.
usitudhaniye watanzania niwajinga sisi eti tumekalia ujamaa na sheria za kazi hatuzijua nyinyi wadau wawili mlio kalia ubepari na nahisi mko marekani basi mbona hamdhaminiki hukuo mlipo? mnafanya kazi kama watumwa at the end of the day mnajiona mmepata kumbe mmepatikani kisawa sawa na hata thamani ya utu wenu hamna.
watanzania tukimuona mwenzetu ananyanyasika badala ya kumshauri vizuri tunazidi kumtupia madongo na kumdidimiza ili ateketee au afee kabisa.Na kujiona sisi ni wajuajie na wasomi,USOMI MWINGI UMELETA WIZI MWINGI DUNIANI.
Kama taalumu zenu za ualimu hebu siku mmoja nendeni katika shule hii anayofundisha mwalimu Daniel Urioh mkafanye kazi kama mnajidai mnajua sheria na kanuni za kazi.Jaribuni kama kweli wababe.
Watanzania tumekuwa bendera kila upepo unapopepea sisi tunafuata shida zetu ndo zinatupelekea pabaya sana na kuwafanya hawa wawekezaji kutudharau,kutupuuza na kuto kudhamin utu wetu na utaifa wetu.
Kwa mfano ukisomeya udoktari urusi,uchina, ujapan,uturuki etc nilazima usomee lugha yao ya taifa kwanza na ukifeli hiyo lugha yao utarudia tena na ukifeli hutoendelea vizuri na shule mbeleni.Tizama wanavyo jali lugha yao na siku za holiday ya nchi yao.watanzania mliopo marekani au popote pale kafunguweni shule zenu na msifuate sheria za nchi hizo mtakiona cha mtema kuni.
mnasema serikali dhaifu; si tumeidhofisha wenyewe,MJENGA NCHI NI MWANANCH NA MVUNJA NCHI NI MWANANCHI. MAFISADI wanaifisidi SERIKALI KWA MBINU ZA MAKUSUDI ILI SERIKALI ISITAWALIKE KISA ANAYETAWALA NI WADINI INGINE.
na kwa taarifa zenu nyinyi wadau hapo juu mliio mtusi mwalimu Daniel Urioh eti ana mambo ya ujamaa,ujamaa huo huo ndo uliokuleeni hadi mkafika hapo mlipo na kujifanya majabar/vidume au vijeke vya mbegu hata kama familia zenu zimekimbilia nchi za njee mngekuwa mmelelewa kibepari bepari kama mlivyo hivi sasa kwa kuishi nchi hizo mngekuwa mnatamani sana kuwa wazungu bahati mbaya sana ndo tuko ngozi nyeusi so inatubidi tuwabudu wao na kufyata mikia yetu kila wakisemacho ni sawa Japo kuwa zitatudhalilisha ni sawa kwa vile ni sheria za kanuni za kazi na kila kilicho choa ni kizuri japo kuwa ni dhaifu. Ndo tulipofikia ni hapa na tunamuona mtanzania mwenzetu hana maana eti ana mambo ya kijamaa na hajui kanuni za kazi,kumbuka ni mwalimu yeye.shida ya ajiri nchini mwetu inatufanya tudhalilike kweli hii haki?
Tungekuwa hatujapitia katika mikono ya walimu tungekuwa/Tungefika hapa tulipo?,mwalimu nyerere si amesoma na kupata udoktorate mbona hakuchagua tittle hiyo kasisitiza aitwe Mwalimu.Kwa sababu kajua ualimu ni fani ya pekee. Leo hii hatuwadhamini walimu wetu na taaluma hii kwa nini kuwe na tafauti, mwalimu nyerere si alikuwa mwalimu yeye au yeye ni wa pekee hakuna kama yeye?
UZENI UTU WENU NA NCHI YENU KWA WAZUNGU HALAFU MNASEMA TUMEKOSA NINI SISI NGOZI NYEUSI KUMBE SELF CONFIDENCE HAMNA HATA KIDOGO KAZI KUABUDU PESA NA KILA CHA MZUNGU.MNAELIMISHWA NA SHERIA ZOTE ZA ULIMWENGUNI ZIMETUNGWA NA WAO KWA MASLAHI YAO ILI DAIMA NGOZI NYEUSI IWE INAWATUMIKIA WAO KAENI MKILIFAHAMU HILI.
POLE SANA MWALIMU DANIEL URIOH JAPO KUWA POLE HASAIDI.LAKINI MUNGU DAIMA YUKO NA WEWE AMIN.
Hivi huyu jamaaa anayelalamika hapa ni comedian ? simuelewi, Eti uzalendo gharama? uzalendo gani? wa kutofuata sheria? unachekesha sana! Hivi bado tuna watu wa namna hii nchini? kweli Kikwete ana kazi kubwa ya kuongoza nchi. Kwani kiingereza hakileti amani? Hiyo wizara ya elimu unayoipa ushauri sijui itakuwa ya nchi gani?
ufanyaji kazi wowote duniani unategemea uwe na nidhamu, sasa bw. Urio kama nimekupa kazi halafu nikakwambia usifanye haya yafuatayo,ukafanya je ukifukuzwa kazi utapinga? Wewe anon unayemtetea huyo mwalimu jaribu kutoa pointi za maana bila ya kutumia jazba na maneno mengi yasiyo na maana. Duniani ya leo imetawaliwa na utandawazi na hao unaowaita mabepari ndiyo wanaongoza hizo institutions, mwenyewe si umeona ujamaa umekufa? Tanzania tunatakiwa tufanye kazi sana na kwa nidhamu kubwa sana kama tunataka kufanikiwa hakuna zaidi, vinginevyo tutabakia hapo hapo tulipo wakati wengine wanaendelea mbele. Binafsi namuonea huruma huyo mwalimu lakini anatakiwa ajifunze kuwa mwadilifu na mtiifu kwa mwajiri wake, huwezi kubishana na mwajiri wako katika sekta binafsi, mwajiri anaweza simply akakukataa, je utafanya nini? hiyo siyo kazi ya serikali au mashirika ya umma. Tuwe wakweli...wala usiwadharau watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi hata kidogo wamejitahidi na wengi wamefika mbali kwa ajili ya nidhamu ya kazi ambayo hatukujengwa nayo kutokana na siasa tuliyoikuta ambayo sisemi ilikuwa mbaya sana lakini leo kila mahali kumebadilika, Hivyo huwezi kuona jinsi wachina wanavyofanya kazi kwa nidhamu na jinsi kunavyokuwa na ufanisi mkubwa?
je picha zina zalisha pesa kwa vipi?
wewe ngoja nikujibu pichazinazalishwa kwawewe kuonyeshaumasikiniwako,kuongea kiswahili nilugha yetu,kamoni=======?
wewe kuwaumeshatembea,lakininazani tembea ujionee wewe hukobongo mtu anakwambia usizungumze kiswahili?
Nakushukuru sana mchangiaji kwa kuwakaripia hawa ndugu zetu wanaofanya kazi huko Marekani kwa kutokutambua uzawa kwanza.
Kwanza kabisa kama ningekuwa mwanasiasa ningemuunga mkono mchungaji Christopher Mtikila na sera zake za uzawa. Nasema hivyo kwasababu wakati Mheshimiwa Mtikila anazungumzia Uzawa ni watanzania wachache sana waliomwelewa.
Lakini ukweli wa neno hilo umetafriwa na msemaji aliyepita alipotoa mfano wa mwanafunzi wa udaktari anapokwenda kuchukua mafunzo katika nchi zinazotumia lugha tofauti na kiingereza.
Amegusia uzawa kwa nchi hizo kutaka kujifunza lugha ya kwao kwanza. Mimi naenda mbali zaidi katika nchi kama marekani kama wewe ni daktari , mhasibu , au mtaalamu yoyote na umetoka Tanzania na vyeti vyako/ nondo kama wanavyoziita hakuna mahali popote utapata ajira kwa vyeti hivyo ni lazima uingie kwenye vyuo vyao
Tumeona swala la ajira kwa wawekezaji kama alivyosema Urio kuwa familia nzima ipo kwenye menejiment bila kujali elimu walio nayo na serikali inakaa kama haioni. Angekuwepo Mtikila kwanza wakurugenzi wangekuwa wazawa wenye vyeti vinavyolingana na stahili ya uwekezaji huo.
Kama alivosema urio watu wenye rangi nyeusi tumekuwa tunawaogopa watu wenye rangi nyeupe siyo tu hapo Tanzania hata huku ughaibuni wanafanya kama wao ni mungu watu kwa rangi nyeusi
Pamoja na kuwa ni sekta binafsi ni lazima kuheshimu sheria za nchi zilizopo , na kama alivyosema mheshimiwa Raisi alivyokuwa anazungumzia raslimali za nchi hususan gesi ni wakati umefika sheria zitungwe kwa maslahi ya watanzania na sio wageni ili watanzania kunufaika na raslimali zetu katika secta zote, ziwe binafsi au serekalini
Msemaji aliyepita amezungumzia mshahara duni ni kweli kwani hizo dola chache wanazolipa hazikidhi zaidi ya kulipa kodi ya chumba kama unataka maisha mazuzi zaidi ufanye kazi mbili hadi tatu na hatimaye kukaribisha kifo mapema kwa kukosa usingizi
Serikali ikisimamia vizuri sekta binafsi hatimaye watanzania tulioko ughaibuni tutarudi nyumbani kuja kufanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ili kujenga nchi yetu.
Nchi hizi za ughaibuni zinapendeza kwa vile wameiba sana raslimali zetu ni wakati sasa kupinga kwa nguvu zote mipango mibovu ya uwekezaji wao kwani tumeshagundua janja yao
Kwa kusimamia haki ni sharti mwalimu Uriyo arudishwe kazini na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wanahusika kwa aliyo yataja.
Mungu ibariki Tanzania dumisha amani na upendo kwa watu wote wenyeji na wageni
Post a Comment