Thursday, August 9, 2012

Mwanafunzi chuo kikuu MIST Mbeya avumbua kifaa cha kudhibiti ajali za meli baharini


Kifaa hiki ndicho kilichgunduliwa bado hakijapewa jina


Mtaalamu maswala ya umeme Joseph Matwani akiwaelezea baadhi ya wananchi waliotembele banda hilo jinzi kifaa hicho kinavyofanyakazi



MWANAFUNZI wa Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MIST) amebuni  na kutengeneza kifaa maalum kinachodaiwa kuweza kudhibiti kupunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa tatizo la ajali za vyombo vya usafiri wa bahari kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Meli ya Mv.Skargit iliyogharimu maisha ya watanzania wengi.

Akizungumza na Mbeya yetu Mtaalamu wa masuala ya umeme katika chuo hicho,Joseph Matwani amemtaja mwanafunzi aliyekitengeneza kifaa hicho ambacho kinabaini meli ama boti litakalozidisha abiria ama mizigo  kuwa ni Zuberi Rutumbo.

Bw.Matwani alisema kifaa hicho ambacho bado akijapewa jina kitakuwa na uwezo wa kutoa taarifa katika mamlaka husika mathalani,Sumatra,Polisi,kwa mmiliki,nahodha na mamlaka nyinginezo zitakazoingizwa katika programu maalum kuwa meli Fulani imejaza mzigo kuliko uwezo wake na hivyo kusaidia kuizuia bandarini kabla haijaondoka.

Mtaalamu huyo amesema kuwa kifaa hicho kitafungwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri wa baharini  ambapo vitawaonesha makapteni kuona kiasi cha mzigo uliopakiwa na kuwajulisha endapo watazidisha baada ya maji kuvuka mstari wa chombo husikai kabla ya kuondoka na hivyo  kutoa mlio wa taadhari na baada ya sekunde kumia ujumbe unakwenda katika nambari za simu zilizokuwa zimefanyiwa programu katika kadi ya simu
.
Amesema kutokana na taarifa hiyo ya ujmbe mfupi wa maneno katika simu za wahusika wanatumaini kuwa watachukuwa hatua kukizuia chombo hicho kisiondoke na hivyo kufanikiwa kunusuru maisha ya  abiria na kupunguza ajali zinazodaiwa zinasababishwa na uzembe wa makapteni kuzidisha mzigo kwa makusudi.

 Mvumbuzi huyo Rutumbo amesema ameamua kutengeneza kifaa hicho alichoanza kukifikiria tangu mwaka 2011  baada ya  kuibuka kwa ajali  mbaya za meli ya Mv.Bukoba,Mv.Spice  na juzi Mv.Skargit na hivyo kuamua kuandika ‘project’ ( mradi) baada ya kushuhudia matukio hayo.

Amesema ajali nyingi zinaonekana zinasababishwa na uzembe wa watu wachache waio na huruma na watanzania lakini anaamini kupitia kifaa hicho uwajibikaji utaongezeka na kila mmoja atawajibika kupitia nafasi yake na kuwabaini wazembe ambapo pia kifaa hicho kinaweza kufungwa  katika mlango ama dirisha katika nyumba na kuprogramu katika simu na hivyo kukupa taarifa ya uhalifu endapo unatokea.

2 comments:

  1. sasa tusiite kuvumbua kwani wazungu wanavyo siku nyingi sana tu, tuseme kaweza kutengeza kutumia njia ya kuunganisha unganisha isiyo ya kitaalam zaidi.
    uvumbuzi ni pale ambapo kitu hicho ni cha kipekee na hakijawahi kutokea.

    ReplyDelete
  2. Hongera na pongezi zimfikie mwanafunzi huyu kwa kuvumbua kifaa kipya tena katika kipindi cha uhitaji mkubwa kutokana na takwimu za ajali za majini kuongezeka.Haya ni maarifa makubwa kwa ngazi yako na kwa taifa pia.Watu kama hawa wanatakiwa kuwa recognized na pia vipaji vyao viendelezwe kwa gharama yoyote.Nchi zilizoendelea walianza hivi na ndio maana hata sasa watu wenye vipaji maalumu wamekuwa wakinunuliwa kwa njia nyingi ili kufanikisha nchi zilizoendelea ni wakati wetu sasa kuthamini vipaji hivi kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake