Mshambuliaji Emmanuel Okwi jana alitangazwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Simba, huku beki Shomary Kapombe akitwaa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu wakati wa tamasha la Simba Day ambalo lilitiwa doa na kipigo cha Simba cha 3-1 dhidi ya Nairobi City Stars ya Kenya katika mechi yao ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Simba ililitumia tamasha hilo la kila mwaka kuwatambulisha nyota wao wapya akiwamo Ramadhani Chombo 'Redondo' aliyejiunga wiki hii akitokea Azam FC ambaye alikabidhiwa jezi Na.6, Mrisho Ngassa aliyetokea Azam pia na beki Mbuyi Twite aliyepewa jezi Na.4 baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea APR ya Rwanda baada ya kupewa dau la dola 30,000 (sawa na Sh. milioni 48).
Wachezaji wengine wapya waliotambulishwa jana ni pamoja na Kanu Mbiyavanga, Salim Kinje, Danny Mrwanda na Kiggi Makasi.
Lakini kulikuwa na shangwe kubwa sana wakati alipotangazwa mshambuliaji Okwi, ambaye alisemekana kuwa mbioni kuiacha klabu hiyo kutimkia Austria kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Red Bull Salzburg na huku pia taarifa nyingine zikidai kuwa alikuwa akijiandaa kujiunga na mahasimu Yanga.
Simba pia walitambulisha jezi zao mpya za msimu huu ambazo walisema kwamba wataziuza wenyewe ili kuiongezea klabu mapato.
Marehemu Patrick Mafisango alipewa tuzo ya heshima ambayo ilipokewa na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Goefrey Kaburu 'Nyange' kwa niaba ya marehemu, huku pia mwanachama mkongwe mwenye kadi Na.3, Profesa Philemon Sarungi akipewa tuzo ya Mchango Mkubwa Kwa Klabu.
Tamasha la Simba Day lilipambwa na mechi ya timu ya wanawake wa klabu hiyo, Simba Queens ambayo mapema iliisambaratisha timu ya Ever Green ya Temeke kwa mabao 5-3 kabla ya kaka zao kulala katika mechi yao dhidi ya City Stars.
Katika mechi hiyo, Simba ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 15 kupitia kwa Mzambia Felix Sunzu aliyemzidi nguvu beki wa City Stars kabla ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa timu hiyo ya Kenya.
Huku ikiwachezesha nyota wake wote wakiwamo wapya, isipokuwa Okwi ambaye hakuwa 'fiti', Simba iliruhusu goli la kusawazisha katika dakika ya 58 kupitia kwa Isancan Owite aliyefunga kwa kichwa na dakika sita baadaye Bruno Okuli aliifungia Stars goli la pili.
Boniface Oryango aliwafungia wageni goli la tatu katika dakika ya 79 akitumia udhaifu wa mabeki wa Simba kushindwa kujipanga na kuishushia Simba kipigo cha pili mfululizo katika siku yao kubwa baada ya mwaka jana pia kulala 1-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya pia.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake