Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Tanzania imeapa kulinda mipaka yake kwa gharama yoyote na kuzionya ndege zozote za makampuni yanayofanya utafiti wa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa kuruka kwenye anga la ziwa hilo, kuanzia jana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alitangaza onyo hilo bungeni jana alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2012/13.
Waziri Membe alitoa kauli hiyo kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Patrick Kabambe, ya wiki iliyopita kwamba ziwa hilo linamilikiwa na nchi yake kwa asilimia 100.
Kabambe alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akieleza kwamba hawana sababu ya kusitisha utafiti wa mafuta na gesi kwa kuwa Malawi ndiye mmiliki wa ziwa Nyasa.
Hata hivyo, mikataba ya kimataifa na mipaka ya wakoloni inaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi upo katikati ya ziwa hivyo asilimia 50 ya ziwa hilo ipo Tanzania.
Membe alisema tatizo lililopo ni kwamba Malawi wanadai kuwa mpaka baina yake na Tanzania unapita pwani ya ziwa hilo; hivyo ziwa lote kutoka kwenye mpaka kati ya Malawi na Msumbiji hadi Kyela, Tanzania ni mali ya nchi hiyo.
Alisema Malawi wanajenga hoja kwa kuangalia mkataba uliowekwa na Waingereza na Wajerumani mwaka 1890 wa Anglo-German Agreeement ulioweka mpaka kati ya Tanzania na pwani ya Malawi.
Alisema Tanzania kwa upande wake inadai kwamba mpaka unapita katikati ya Ziwa kutoka mpaka wa Malawi na Msumbiji usawa wa latitudi nyuzi 9 na 11 hivyo kufanya eneo lote la Kaskazini Mashariki kuwa mali ya Tanzania.
Alisema Tanzania inazo ramani na mipaka iliyotengenezwa na wakoloni wa Kiingereza waliotawala Tanganyika na Malawi ambao walikubaliana kurekebisha mpaka na hivyo kuusogeza hadi katikati ya ziwa kama ilivyo kwa Malawi na Msumbiji.
Alisema baada ya kuibuka kwa tofauti hizo, ilikubalika kwamba pande zote zikutane ili kumaliza mgogoro huo kwa njia ya diplomasia.
Alisema tatizo la mpaka kwa Tanzania si la kwanza na katika mengine imefanikiwa kuyamaliza ikiwemo ule wa bahari kati yake na Comoro na Msumbiji, ambao ulimalizika Desemba mwaka jana.
Alisema mpaka mwingine ni ule uliobadilishwa Februari 17, mwaka huu, ambapo Tanzania ilikaa na Ushelisheli na pande zote zilibalisha mpaka wa Tanzania baharini.
Alisema katika mgogoro wa Malawi, madai ya Tanzania yanakuwa na nguvu kwa sababu ya kulinganisha mzozo kati ya Cameron na Nigeria kuhusu mpaka wa ziwa Chad ambao ulipelekwa Mahakama ya Kimataifa (International Court of Justice) na kuamuriwa kuwa mpaka huo upite katikati ya ziwa Chad katika mstari ulionyooka.
Alisema uamuzi huo ulitokana na sheria za kimataifa zinazoeleza pamoja na mambo mengine kwamba mstari ulionyooka upitao katikati ya ziwa ndio mpaka halali kati ya nchi na nchi ikiwa zitapakana na ziwa.
”Kutokana na maelezo haya yote, ni dhahiri kuwa tunalo tatizo linalohitaji kutatuliwa kati yetu na Malawi juu ya mpaka wa ziwa Nyasa,” alisema Membe.
Alisema tatizo la mpaka kati ya nchi hizo mbili lisingeweza kutatuliwa miaka ya nyuma kwa kuwa kiongozi wa Malawi wakati huo, Dk. Kamuzu Banda alikuwa rafiki wa serikali ya makaburu wa Afrika Kusini wakati Tanzania ilikuwa ikiunga mkono harakati za wapigania ukombozi wa watu weusi waliokuwa wakidai uhuru nchini humo.
Alisema Tanzania pia ilikuwa makao makuu ya vyama vya wapigania haki duniani hivyo wapinzani wa Malawi walikimbilia Tanzania jambo lililomfanya Banda aamini kwamba Tanzania ilikuwa kichaka cha maadui wa serikali yake.
”Haya hayakuwa mazingira mazuri ya kutatua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi kwa wakati huo,” alisema.
Membe alisema baada ya utawala wa Banda kuondoka, utawala wa Bakili Muluzi, Bingu wa Mutharika na sasa Joyce Banda, umeimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Malawi umeimarika kiasi cha kuruhusu majadiliano ya kumaliza mgogoro huo.
Alisema mwaka 2005, Mutharika alimwandikia Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akimtaka waunde kamati ya kuangalia tatizo hilo ili kulipatia ufumbuzi.
Alisema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, alikutana na Mutharika mara mbili na wakakubaliana kuanzisha tume za kushughulikia tatizo hilo chini ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo.
Alisema timu ziliundwa na zilianza kukutana tangu mwaka 2010 na kuandaa hadidu za rejea kwa ajili kushughulikia tatizo hilo la mpaka ikiwemo kukusanya nyaraka mbalimbali.
Membe alisema mazungumzo yalikuwa yanaendelea, lakini katika hali ya kushangaza, Serikali ilipata taarifa za kuaminika kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwamba serikali ya Malawi imetoa eneo lote la ziwa Nyasa kama vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi.
Aidha, alisema makampuni yanayofanya utafiti huo ziliomba kibali cha kurusha ndege zake lakini Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikataa.
”Pamoja na katazo hilo, serikali yetu ilipata ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti, zenye uwezo wa kutua majini na nchi kavu zinazokadiriwa kuwa tano zilionekana zikivinjari na kutua ziwa Nyasa katika upande wa Tanzania na kwenye ufukwe wake hayo yametokea kati ya Januari 29 na Julai 2, mwaka huu,” alisema.
Alisema: “Baada ya majadiliano ya makubwa baina yetu na Malawi, serikali yetu iliwataka wenzetu wa serikali ya Malawi pamoja na kampuni za utafiti au uchimbaji kusitisha mara moja shughuli zote za utafiti hadi majadiliano yatakapokamilika.”
Alisema baada ya matukio hayo, Tanzania iliwasiliana na serikali ya Malawi kwa maandishi na kuita mkutano wa kujadili hali hiyo na mustakabali wa mpaka huo uliofanyika Julai 27 na 28 jijini Dar es Salaam na pande zote zilikubaliana kwamba lipo tatizo baada ya kila mmoja kushikilia msimamo wake.
Alisema walikubaliana kwamba mkutano wa wataalamu na baadaye wa mawaziri wa mambo ya nje ufanyike nchini Malawi ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Alisema serikali ya Tanzania iliitaka serikali ya Malawi kutoruhusu kampuni yoyote kuendelea na utafiti kwa kuwa kufanya hivyo kungeathiri majadiliano.
”Serikali ya Tanzania inathamini uhusiano uliopo baina ya nchi mbili na ina dhamira ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema kwa manufaa ya watu wetu,” alisema.
Aliitaka serikali ya Malawi kuheshimu makubaliano ya Julai 27, mwaka huu kwa kuwa nia nzuri ya kutatua mgogoro baina yao ni mazungumzo ya amani.
Aliionya Serikali ya Malawi kutoruhusu mtu, kikundi au kampuni yoyote kufanya utafiti au uchimbaji kaskazini mwa ziwa Nyasa kwa kuwa majadiliano ya mpaka yanaendelea.
Alisema kuna Watanzania takribani 600,000 wanaotegemea ziwa Nyasa kiuchumi na kama chanzo cha uhai wao hivyo serikali itawalinda.
”Serikali ya Tanzania inapenda kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayofanya shughuli za utafiti kwenye eneo hilo linalobishaniwa kuanzia leo Jumatatu (jana), kuacha shughuli zao, serikali haitaruhusu utafiti huu kuendelea hadi makubaliano na majadiliano kuhusu mpaka yatakapofikiwa kati ya nchi zetu, tuipe diplomasia nafasi,” alisema.
Waziri Membe aliwataka wananchi wanaozunguka ziwa Nyasa kuendelea na shughuli zao za kiuchumi bila wasiwasi wowote kwa kuwa serikali iko macho, ipo imara na ipo tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote.
”Chini ya uongozi wa serikali ya CCM wananchi wa Tanzania daima watakuwa salama dhidi ya tishio lolote la dhahiri au la kificho la kiusalama, tumefanya hivyo tokea uhuru na hatutachelea kufanya vinginevyo wakati wote tukiwa madarakani,” alisema.
Hata hivyo, alisema upo uwezekano mkubwa wa mgogoro huo kutatuliwa na msuluhishi badala ya Tanzania na Malawi.
Wakati Membe akitoa taarifa hiyo, na ujumbe wa kamisheni ya utumishi wa Bunge la Malawi, ulioongozwa na Naibu Spika wa Bunge hilo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere.
Septemba mwaka jana, aliyekuwa Rais wa Malawi, hayati Bingu wa Mutharika, aliridhia kampuni ya Surestream Petroleum ya Uingereza, kupewa leseni ya kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye kina kirefu cha ziwa hilo na tayari kampuni hiyo imeanza kufanya utafiti wa athari za mazingira za mradi huo.
Ziwa Nyasa lina ukubwa wa kilometa za mraba 29,600 ambalo ni la tatu kwa ukubwa kati ya maziwa ya maji baridi barani Afrika.

CHANZO: NIPASHE
na bado hii sakala litazidi heko heko malawi daini chenu mpaka kieleweke
ReplyDelete