Saturday, August 11, 2012

PAPA MSOFE ASEKWA MAHABUSU KWA KOSA LA MAUAJI

 Marijani Abubakar Msofe ‘Papaa Musofe’ (58) akiingia kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, kwa ajili ya kusomewa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili
Papaa Musofe wa pili kulia, akiwa amekaa kwenye gari ya polisi chini ya uangalizi mkali, tayari kwa safari ya kurudi mahabusu.Picha Zote na Mdau Francis Dande
Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Abubakari ama Papa Msofe (50), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la mauaji.

Papa Msofe Mkazi wa Mikocheni, alisomewa shtaka lake jana mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome wa mahakama hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka, alidai kuwa Novemba 6, mwaka 2011, eneo Magomeni Mapipa, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kumuua Onesphoty Kitoli.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji hadi upelelezi utakapokamilika, kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania.

Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutaja.

Hakimu Mchome alisema kesi hiyo itatajwa Agosti 23, mwaka huu na mshtakiwa apelekwe mahabusu.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake