Saturday, August 11, 2012

USAIN BOLT: BINADAMU MWENYE KASI ZAIDI DUNIANI - NA MWANARIADHA ANAYETENGENEZA FEDHA NYINGI ZAIDI KULIKO WOTE KATIKA HISTORIA


 

Wakati zawadi ya fedha ni kidogo, fedha anayopokea Usain Bolt kwa siku ni kubwa shukrani kwa kwa malipo anayoyapata kwa kila anapocheza. Gharama zake kwa kila anapocheza zinaanzia £200,000 na zinaweza kufikia £350,000 kutokana na mchuano wenyewe. Bolt ana demand malipo makubwa kwa sababu uwepo wake kwenye mchuano unatoa guarantee ya uuzwaji wa tiketi zote.


"Bolt ndio mchezaji anayelipwa vizuri kuliko wote katika historia ya mchezo huu wa riadhaa, lakini pia inawezekana ndio anayelipwa kiasi kidogo sana kwenye historia ya mchezo, anasema Paul Doyle, wakala wa muda mrefu wa mchezo wa riadha, katika story ya Bolt iliyotolewa katika Sport Illustrated.

Uwepo wake katika mashindano ya Penn Relays mwaka 2010 ulipelekea idadi kubwa zaidi ya mashabiki kuhudhuria uwanjani walikuwepo watu 54,310 ikiwa ni historia kwa Penn Relays inayofanyika tangu miaka 118 iliyopita.

Bolt anastahili kulipwa vizuri zaidi kwa sababu amebadilisha upepo wa mchezo, kama Tiger Woods alivyofanya kwenye gofu na Micheal Jordan alivyofanya kwenye kikapu.

Wakati wa olympic mwaka huu, siku ilipofanyika fainali ya riadha mita 100, waandaji wa London Olympic 2012 walipata maombi zaidi ya watu millioni 1 kwa ajili ya tiketi kwa gharama ya $1,130, tiketi ya ghali zaidi kuliko mchezo wowote kwenye michezo hiyo inayoendelea huko London.  Bolt alikuwa na ushindani mkali na mjamaica mwenzie Yohan Blake, ambaye ni bingwa wa dunia wa mbio za mita 100, baada ya Bolt kuondolewa kwenye mbio za mwaka uliopita kwa kucheza ndivyo sivyo. Blake pia alimshinda Bolt kwenye mashindano ya majaribio ya mbio huko Jamaica.

Bolt alimshinda Blake kwenye mbio za mita za Olympic jumapili iliyopita akiweka rekodi mpya ya kukimbia kwa muda mfupi zaidi ikiwa ni 9.63 seconds. Anaungana na Carl Lewis kuwa binadamu pekee kushinda mfululizo medali za dhahabu katika mbio za wanaume za mita 100.

Akiendelea kushikilia ubingwa jina lake la utani kama binadamu mwenye kasi zaidi duniani, atakuwa na uwezo wa kuendelea kutaka kulipwa fedha nyingi kupitia ada yake ya kushiriki mashindano pamoja na mikataba ya matangazo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake