Jay'z ni mwanamuzic mwenye mafanikio makubwa sana, mafanikio yake yametokana na jinsi anavyoweza kujiingiza katika biahashara mbali mbali. Ukiachia muziki wake pia anabiashara zingine nyingi zinazo mwingizia pesa. Mimi na wewe hatuezi kuzijua zote lakini kuna hizi tatu music, nguo na sasa kuwa mmiliki wa timu ya mpira wa vikapu (basketball) inayojulikana New Jersey Nets akishirikia na tajiri mkubwa sana anaejulikana kwa jina la Mikhail D Prokhorov kutoka Russia na wameweza kuihamisha timu hiyo kutoka New Jersey hadi Brooklyn New York, na kuibadilisha jina baada ya kuitwa New Jersey Nets na sasa timu inajulikana kwa jina la Brooklyn Nets. Hapa chini ni picha ya sehemu ya uwanja maeneo ya down town Brooklyn.
Picha hii ni uwanja huo ukiwa katika matengenezo ya mwisha hadi ifikapo sepetember utakuwa umekamilika na utakuwa tayari kwa kutumiwa na michezo yake ya nyumbani ya time ya Brookyl Nets kama itakavyo julikana. Pita pita ya Vijimambo ilipata ukodak huu live katika eneo hilo la down town Brooklyn maarufu kama Jay Street.
Picha hii ni down town Brooklyn, Ny
Uwanja utakavyo onekana baada ya kukamilika na unaweza kuona alama na number husika za usafiri wa garimoshi (treni) au maarufu kwa jina la Subway, garimoshi zitakazo pita hapa kama ukibahatika kutembelea New York na kutaka kwenda kuona uwanja huu unaeza kutumia garimoshi zenye alama hizo hapo juu. Gharama za ujenzi wa uwanja huu hadi unakamilika ni billion 1.
Sehemu ya kuchezea itakavyo onekana kwa ndani, kwahiyo New York kutakuwa na time mbili za basketball New York Knicks yenye kutumia uwanja wa nyumbani Madison Square Garden uwanja uliopo Midtown Manhattan na Brooklyn Nets uwanja utakuwa Down town Brooklyn, NY.
|
Uwanja huu pia utakuwa unatumika kwa mchezo wa magongo wa barafu (Ice hockey), huu ni mchezo unaochezwa juu ya barafu ingawa hadi sasa sijajua ni timu gani itautumia uwanja huu kwa upande wa mpira wa magongo, na pia utatumika kwa matamasha mbali mbali. Kwa upande wa Vikapu uwanja huu utakuwa na uwezo wa kukalisha watu 18,103, na kwa magongo (Ice hockey) watu 14,500, na utakavyo tumika kwa matamasha utaweza kuchukua watu 19,000. |
|
Ukitaka kuendesha kufika hapa unaeza kutumia daraja la Brooklyn Bridge kama uonavyo au kwa mbali unaona Mahattan Bridge, Mambo ya New York hayo na Ny Ebra wa vijimambo. |
Umenikumbusha mbaaali Ny Ebra wa vijithings, ulinipitisha hayo maeneo.
ReplyDeleteMdau wa Ulaya