Friday, August 10, 2012

SHUKRANI

Habiba na farida jetha tunatoa shukrani za dhati kwa wote mliofika kwenye Hitma ya kaka yetu mpendwa iliyofanyika Jumamtano Aug 8, 2012 nyumbani, Silver Spring.

Taarfia tumetoa ilikua ni ya muda mfupi lakini mlijitokeza kwa wingi kujumuika na sisi katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kaka yetu mpendwa, kusema ukweli tumefarijika sana .

Hatuna neno la shukrani litakalolingana na mlichotufanyia zaidi ya kusema asante. mmetutia nguvu, kutupa moyo na kujisikia mpo pamoja nasi kama ndugu wa baba  na mama mmoja.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema awazidishie maradufu. Asante.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake