Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta,
Uhusiano kati ya Tanzania na Malawi upo hatarini baada ya serikali ya Malawi kutangaza kwamba ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa asilimia 100 ilhali sehemu ya ziwa ipo Tanzania.
Mbunge wa Mbozi Magharibi (CCM), Godfrey Zambi, aliliambia Bunge jana alipoomba mwongozo wa Spika akieleza kuwa vyombo vya habari vya Malawi na vya Tanzania vimemkariri mmoja wa makatibu wakuu wa Malawi, akieleza kwamba ziwa Nyasa lipo nchi mwake kwa asilimia mia, hali ambayo inahatarisha uhusiano wa nchi hizo.
“Ni vyema serikali ikatoa maelezo juu ya hali ya ziwa Nyasa ili wananchi wa Mbeya na wabunge hapa tuelewe, maana kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mpaka wa ziwa hili na hatujui kilichofikiwa,” alisema.
Alisema taarifa za katibu huyo zinatia wasiwasi na hofu kwa wananchi wa Mbeya ambao wanatumia ziwa hilo kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama, alisema suala hilo atalipeleka serikalini ili Waziri Mkuu au Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alitolee ufafanuzi na taarifa kamili.
Hata hivyo, Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta, alisema serikali imestushwa sana na taarifa hizo kwa kuwa mazungumzo kuhusu mpaka wa ziwa Nyasa yanaendelea.
Alionya kwamba Tanzania ipo tayari kwa uchokozi wowote kwa kuwa inafuata sheria za kimataifa, hivyo akawataka wananchi wa mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Iringa, ambayo inapakana na ziwa hilo kuendelea na shughuli zao za kiuchumi ziwani humo.
Alisema kauli rasmi ya serikali kuhusu jambo hilo itatolewa bungeni Jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wakati huo huo, ratiba mpya ya Bunge inaonyesha kwamba Mkutano wa Nane unaoendelea sasa utamalizika Agosti 16 badala ya 22 iliyokuwa imepangwa awali ili kutoa fursa kwa wabunge Waislamu kwenda kusherekea sikukuu ya Idd na familia zao.

CHANZO: NIPASHE
3 comments:
haya haya zulma mnayo wafanyia watu wa visiwani sasa ina backfire kwenu malawi oyee daini ziwa lenu hilo haya haya,rahman(mwenyezi mungu) ameshashema wazi kabisa HATOZIDISHIWA KITU AFANYAYE ZULMAA.
MALAWI THIS IS THE GOOD ONE HA HA HA
Jamaa hapo juu naona unamuhusisha Mwenyezi mungu kwa mambo ya watu binafsi wenye tamaa,Visiwani wanadhudhulma gani wanafanyiwa wa visiwani , kama sio wao kuitumia tu bara?wa bara hatufaidiki na lolote na muungano huo,kumbuka kuwa hizo neema za utalii zimetokea Mombasa baada ya watu mnaowaamini {Waarabu}kuvuruga Mombasa nakuhamia Zanzibar , kumbuka kuwa hao maharamia watakuja vuruga hata huko je mtakwenda wapi?na sisi muungano hatuutaki tena ufe tuwe na inchi mbili na viza pia,kuhusu ziwa Nyasa unaonekana haujui kitu, hata ramani ya nchi yako,fuatilia miaka ya 78 na 79 kilitokea nini kule kuhusu hicho unachochelea,waliyamaliza na utawala wa Hayati Banda tafuta hilo ndio uje hapa utuandikie.
Huyo anony wa kwanza unahitaji msasa kichwani ndugu yangu, kwanza huko visiwani mna kitu gani cha kudhurumiwa????,mkivunja muungano piga hesabu wazanzibari wangapi wapo bara wananufaika comapared na wabara wangapi walio huko visiwani?,mnakimbilia tu na hoja ya kuvunja muungano hamjui hata mtawaweka wapi watu wenu wakirudishwa kutoka huku bara, mtakaa kwenye magofu mpaka yawahangukie...waarabu wanawadanganya sana, na kwa taharifa yako mkivunja muungano kutakuwa hamna hata hiyo zanzibar,nyie wenyewe kwa wenyewe hampatani mnabaguana bila ya muungano...pemba nao watataka nchi yao.
Hacha kushabikia tu suala la malawi bila ya data na hacha kumtumia mungu kwa vitu ambavyo huvijui utajichotea dhambi bure bila ya sababu ya msingi kwenye mwezi huu wa ramadhani.
Post a Comment