Tito Okello
Stori: Walusanga Ndaki
UKITAKA kuufahamu vyema ‘msululu’ wa marais waliowahi kuitawala Uganda kuanzia kwa Rais Yoweri Museveni wa sasa, hebu soma yafuatayo:
Museveni aliingia madarakani kwa kumpindua mwanajeshi, Tito Okello ambaye naye alichukua nafasi hiyo kutoka kwa mwanajeshi mwenzake, Bazilio Olara-Okello.
Yeye pia alimpindua Milton Obote ambaye naye aliingia madarakani baada ya kuuangusha utawala wa Idi Amin Dada. Amin naye aliingia madarakani kwa kumpindua Milton Obote huyohuyo mwaka 1971.
Kwa ufahamisho tu, kabla ya Obote kurejea madarakani baada ya kuangushwa na Amin, palipita marais watatu wa ‘harakaharaka’ ambao ni Yusuf Kilonde Lule, Godfrey Binaisa na Paul Muwanga, ambao safu hii itawachambua baadaye.
Tito Okello aliingia madarakani Julai 29, 1985 hadi Januari 26, 1986 baada ya kula njama za kumwangusha Obote. Alidumu madarakani miezi sita tu, akaangushwa na Museveni na kama kawaida ya wanasiasa wengi wa Uganda wakati huo, Okello alikimbilia Tanzania ambako aliishi kwa muda kabla ya kukimbilia Kenya ambako alifariki dunia Juni 3, 1996 akiwa na umri wa miaka 82.
Okelo alizaliwa 1914, akawa mwanajeshi tangu 1940 wakati wa ukoloni wa Uingereza na alikuwa miongoni mwa askari wa Uganda walioungana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kumwangusha Idi Amin mwaka 1979.
Ndiye Jenerali Tito Lutwa Okello, ambaye baada ya kuingia Ikulu ya Uganda mambo yalizidi kuvurugika, hususan kutokana na kile kilichoelezwa na wachunguzi ‘kisomo chake kidogo’
GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake