Tuesday, August 7, 2012

USAIN BOLT: SITANII, NDOTO YANGU NI KUICHEZEA MAN UNITED - FERGIE ALINIPA OFA YA MAJARIBIO


Imagination - Usain Bolt ndani ya jezi ya United

Binadamu mwenye kasi zaidi duniani Usain Bolt jana alimuomba Sir Alex Ferguson nafasi ya kwa ajili ya kuichezea Manchester United.

Bingwa huyo wa Olympic wa mbio za mita 100 alisema ndoto yake hiyo mara pale alipoulizwa kuhusu changamoto yake inayofuta.

Bolt mwenye miaka 25 alisema: " Watu wanadhani natania. Lakini Sir Alex Ferguson alinipigia na akasema, "OK, njoo na ufanye majaribio" itakuwa haiwezekani kwangu kuipoteza nafasi hii na kukataa.
Usain Bolt na Sir Alex

" Nisingeweza kuikubali changamoto hii kama ningefikiri sikuwa mzuri kiasi cha kuiweza. Mimi ni mchezaji niliyekamilika na naweza kuleta tofauti.

"Nitakuwa mchezaji mwenye kasi zaidi kwenye timu - lakini nikicheza vizuri pia.."

Mjamaica huyo aliongeza: "Nipo hapa Uingereza kwa siku kadhaa, Ikiwa Sir Alex ataniita kwa ajili ya majaribio - anajua namna ya kunipata"
Bolt na medali yake ya dhahabu

Bolt - ambaye juzi alivunja rekdoi ya dunia kwa kukimbia kwa sekunde 9.63 katika ushindi wake wa mbio za mita 100, amekuwa na urafiki na Fergie na wachezaji wake tangu alipotembelea Manchester  2009 wakati alipoenda kwenye mashindano ya mita 150.

Alisema: "Kwa dhati kabisa nataka  kuona nini nitafanya. Nafikiri naweza kuwa kama Rooney."
Kikosi cha Manchester United kitakavyokuwa na Bolt ndani.

Usiku wa jana mashabiki wa klabu hiyo walimsapoti. Adam Haworth, 35, alisema: "Tungeweza kufanya vizuri zaidi kama tungekuwa na mtu mwenye kasi na nguvu msimu uliopita!"

"Chris Hicks, 49, kutoka Manchester, alisema: "Itabidi tumpeleke kwenye timu ya reserves kwa mwaka mmoja ili kumfundisha zaidi, - then wakati Ryan Giggs atakapostaafu tayari tutakuwa na mbadala aliye tayari."

Msemaji wa United alisema: "Kama binadamu mwenye kasi kuliko wote ulimwenguni, kwa hakika ataongeza kasi kwenye timu."


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake