Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso (kushoto) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal,(wa pili kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya uandaaji hadi kukamilika kwa Sukari tayari kwa matumizi,kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Wa tatu kutoka (kushoto) ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake