heilla Sezzy, Mwanza
WANANCHI 1,500 wa jijini Mwanza wanatarajiwa kupimwa na kutibiwa bure, matibabu yanayotolewa na taasisi ya Aga Khan kwa kushirikiana na Bima ya Taifa ya Afya (NHIF).
Matibabu hayo yalianza kutolewa jana Agosti 31 na yanatarajiw akukamilika leo Septemba Mosi, yakiwa na lengo la kutoa fursa kwa wananchi ambao wameshindwa kutibiwa mahospitalini kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu.
Mwenyekiti wa Aga Khan mkoani hapa, Karm Jamali alisema kuwa wananchi wengi wanashindwa kwenda hospitali kwa sababu wanakuwa hawana fedha za vipimo na matibabu.
“Kitu ambacho tunakifanya hapo ni kuwapima wagonjwa, magonjwa ambayo tumeyaainisha kwao na watapata fursa ya kujua hali za magonjwa waliyonayo na kuendelea na matibabu hata katika hospitali za Serikali ambazo zina unafuu wa matibabu,” alisema Jumali.
Alisema kuwa wagonjwa ambao watatakiwa kuendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari watatakiwa kutuma maombi kwa bodi ya Aga Khan ambayo itajadili na kuona jinsi ya kumsaidia mgonjwa huyo kwa kupata matibabu bure.
Aliendelea kwa kusema kuwa huduma hiyo ya vipimo na matibabu itakuwa endelevu ambapo kwa kuanza wameanza na mkoa wa Mwanza na baadae watafika katika mikoa mingine nchini.
“Dawa tunazo za kutosha hivyo wananchi wasihofu. Kwa wale watakaobainika kuwa na magonjwa watapatiwa dawa hapa hapa na wengine watapewa ushauri kutona na magonjwa yao,” alisema.
Jamali alisema kuwa wamekuwa na changamoto kwa wagonjwa wa kisukari ambao wamekuwa wakitumia dawa za asili badala ya za hospitali na wamefika katika kupatiwa vipimo hapo wakiwa katika mbaya.
“Wagonjwa wa aina hiyo tunashindwa kuwatibu kwa sababu, hali wanazokuwa nazo wanatakiwa kwenda katika hospitali ya rufaa, hivyo tunawaomba wagonjwa kutumia dawa za hospitali kwa sababu zina uhakika mkubwa wa kutibu,” alisema Jamali.
Magonjwa ambayo wanapima na kutoa matibabu yake ni malaria, kisukari, shinikizo la damu pamoja na maambukizo ya njia za mkojo.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment