Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Vipaji maalum ya Ilboru wakipata maelezo jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake 21 yanavyofanya kazi, Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa maelezo hayo.
Wanafunzi wa sekondari ya Ilboru wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwenye banda la maonyesho wakati wa mkutano wa 14 wa Mazingira jijini Arusha. Kulia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa UN Sangita Khadka Bista, Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha UN (UNIC) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu.
Meneja Mkuu wa Uwezeshaji wa Shirika la Manedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Ishmael Dodoo akimwongoza Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (wa tatu kulia) alipowasili katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) kuhuduria mkutano wa 14 wa Mazingira na Uzinduzi wa mtandao wa Mazingira unaosimamiwa na NEMC.
Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kulia) akisikiliza Wafanyakazi wa UN Harriet Macha na Katibu wa klabu za Umoja wa Mataifa mkoa wa Kilimanjaro Angaja Fundisha wakitoa maelezo kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Arusha.
Bw. Ishmael Dodoo wa UNDP wakijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa hapa nchini Dr. Alberic Kacou wakishikana mkono na kusalimiana na Dr. Mohamed Abdel-Monem wakati wakisubiri kuingia katika ukumbi wa mkutano wa Mbayuwayu uliopo AICC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal (Kulia) akiwa meza kuu na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoros Dr. Fouad Mohdji (katikati) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wa Mazingira wa Tanzania.
Kwa picha zaidi bofya read more
Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akitoa ripoti juu ya mtandao wa Mazingira utakavyokuwa ukifanya kazi, akifafanua juu ya mtandao huo na moja ya kazi zake kuwa ni kufikisha kwa wananchi habari za mazingira juu ya uharibifu na utengenezaji wa mazingira hapa nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa anaona fahari malengo ya mkutano wa RIO+20 yakifanikiwa na kuyaendeleza mazuri katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kwa sasa kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni na vilevile Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika mapambano hayo na kuweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilail akiangalia jinsi mtandao wa mazingira ulivyopangwa na utakavyofanyakazi baada ya kuuzindua rasmi kwenye ukumbi wa Mbayuwayu mbele ya wataalamu wa Mazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Mtandao huu unapatikana kupitia www.tanzaniaenviroment.go.tz
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akiteta jambo na mmoja wa wadau wa mazingira kutoka NEMC baada ya kuzindua mtandao huo.
Meza kuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka nchi 53 za Afrika kwenye ukumbi wa Simba katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC jijini Arusha.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt. Alberic Kacou akifurahi jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Bw. Abdallah Hamdok.
Pichani Juu na Chini ni Meza za Mawaziri wa Mazingira barani Afrika na viongozi wa Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi wa mkutano 14 wa Mazingira jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Dr. Fouad Mohdji (kushoto) Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ambaye pia ni Rais wa Mazingira Barani Afrika kwa kipindi cha miaka miwili Dkt. Terezya Huvisa (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Makamu wa Rais (hayupo pichani).
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akittoa maelezo ya mwanzo juu ya mkutano 14 wa mazingira mbele ya Makamu wa Rais (hayupo pichani) jijini Arusha.
Rais mstaafu shirikisho la mazingira Afrika (AMCEN) Bw.David Sagara kutoka Mali akizungumza na mawaziri wa Mazingira na kukabidhi kiti kwa nchi ya Tanzania ambapo Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa amepokea Urais huo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dr. Alberic Kacou akielezea amesema huu mkutano wao kama Umoja wa Mataifa ni kuweka misingi na uwezeshaji ambayo inayoletwa na Serikali za mataifa mbalimbali ambao ni wanachama wa Umoja huo juu ya Suala zima la maendeleo na mazingira na changamoto zinazoyakibili mazingira na kusaidia Utawala juu ya swala zima la ardhi ikiwemo misitu kwa ujumla na kuwawezesha fedha juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingira kwa ujumla juu ya utumiaji na utunzaji wa mazingira halisia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akifungua mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira barani Afrika jijini Arusha.
Baadhi ya Wataalamu wa Mazingira wakimsikiliza Makamu wa Rais (hayupo pichani) wakati akifafanua jambo juu suala zima la mazingira na udhibiti ili tuendele kuwa mfano na kuapa zawadi nyingine juu ya utunzaji wa mazingira na gesi ya ukaa ya Ozoni hapa nchini kwetu.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake