ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 7, 2012

FRANCIS GODWIN :NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU. AENDA MAFICHONI AKIHOFIA KIFO KABLA HAJATOA USHAHIDI NA KUSEMA UKWELI WA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI!


Mmiliki wa mtandao huu http://www.francisgodwin.blogspot.comBw.Francis Godwin (kushoto) akitoka kujisalimisha polisi akiwa na mkewe Vumilia Mwangosi (kulia) ambaye ni dadake na marehemu Daudi Mwangosi
Hapa mzee wa matukio daima akiwa na mkewe katika basi
Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa.

Chanzo: Iringa Yetu

3 comments:

Anonymous said...

That nice mtu wangu sema ukweli

Anonymous said...

Tulikuwa tunawacheka wakenya sasa haya mambo ynashamiri kwetu.IGP wacha kuwa unapendelea chama kimoja au kuficha wauaji kwa ajili ya maslahi ya watu wako. Leo upo hapo kwenye kesho haupo kwenye hiyo nafasi utasema nini ukihitajika kutoa ushahidi.Kumbuka wanaokufa ni watu kama wewe na wana wazazi kama wewe.Je mzazi, ndugu au jamaa wako akiuwawa kwenye hiyo mikutano utafanya nini?Nashauri wananchi kuweni macho na hawa askari watawamaliza ndugu zetu kwa ltumiwa na watu wachache,msishirikiane nao kwa lolote lile na pia msitoe msaada wowote kwa jeshi la polisi kwani wameonyesha kuwa wao ni majambazi wa mchana na kutokiuwa na aibu na huruma ya wananchi mbele ya Mungu.kamanda wa mkoa wa iringa na wasadidiz wake wote wanatakiwa wajiuzulu haraka sana na askari waliokuwepo siku ya mauwaji wahojiwe na kamati maalumu ya bunge iwe na washiriki wa vyama vyote na majaji wanne wenye sifa nzuri ya kufuata sheria.Serkali ispofanya hivi basi wajue kuwa wao ndio wahusika wakubwa.Francis usije kudanganywa ukajitokeza bila ya kuwa na watu unaowaamini na pia tengeneza copy nyingi za hizo picha za mwanaharaki mwenzetu na wape ndugu na jamaa wa karibu ili chochote kikitokea kwako wao wanazo na watazitoa kwenye vyombo vinavyohaminika nakuonyesha ukweli.Haikikisha unakuwa na watu kila uendapo na kila ufanyalo upo na watu.Mungu atakulinda Amen

Anonymous said...

Hili swala si dogo serikali isije ikachukulia mchezo,Hakika ukatili huu watalipa tu,hiyo ni damu isiyo na hatia yoyote atakaye tetea uovu huu damu ya huyu mtu itajilipiza.Hili ni tukio la kinyama sana lililofanywa na jeshi la polisi,hawakutenda haki kabisa.Wanapaswa kujua kazi yao ni kulinda wananchi sio kuwaua hivi kweli Tanzania inayotajwa kwa amani inahitaji mabomu ya moto kutuliza ghasia kweli?!natafakari hata haieleweki.Serikali iangalie sana jinsi wanavyoshughulikia hili jambo,hii itaua kabisa imani kwa jeshi la polisi na serikali kwa ujumla.Kuna organization zinajiita za haki za binadamu hapo nyumbani na zimechangiwa mapesa kwa ajili ya cases kama hizi mbona hatuwasikii hata wakisema lolote au ndio hofu imejaa kila sehemu.Hakika demokrasia bado tanzania ni vitisho tu kila sehemu hakuna hata wa kuaminika!Hamuwezi kumuua mtu na kumkanyaga km mnyama bila kujali.We need video clip this killing need to go viral,,Everything is global now,let the world know huu unafiki umezidi sasa!!