Friday, September 14, 2012

JIKUMBUSHE TU UNGEKUWA MITAA HII UNAGANGA NJAA NA MAISHA YA DOLA MOJA KITAA.


 Mwananyamala ukitaka kwenda Sokoni kuangalia vitu vya kununua ili kuweka nyumbani na maisha yaendelee. Pichani hapo juu ni maeneo ya kona ya Mwananyamala kama unatokea Kinondoni na kuelekea Mwananyamala Hosp, hii ni kila siku kunakuwa na foleni na hii inatokana na Daladala kubwa zinazosimama hapo kuchukua abiria na kuweka foleni kwa magari yanayotaka kukata kona. Wale wakitaa hiki naona nimewafikisha kimawazo kona hii.
Kwenye soko la Mwananyamala nyanya fungu linauzwa kwa sh 300 hadi 400 so niliondoka na fungu zangu za 400 zakutosha kwa wiki kadhaa, ndo hadi uwenazo hizo 400 kama hakuna nyumbani mboga chukuchuku.....
Bei ya mchele kama unavyoziona zinaanzia shillingi 1700 hadi 2000 kwa kilo moja, hapo sasa nyumbani wali hauliki hadi sikuku au mgeni aje home sweet home.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake