Friday, September 14, 2012

Jitambue ili kutimiza ndoto yako


TUMEKUTANA katika kona yetu kujuzana mambo machache ambaye yapo katika maisha yetu ya kila siku, hususan katika mapenzi.

Kila kukicha nimekuwa katika nikijitahidi kuwasaidia wenzangu wenye matatizo kutokana na kidogo nilichonacho ili kila mmoja afurahie mapenzi.

Nimerudi tena kwenye mada ya simu ya mkononi, baadhi ya watu wamepoteza uaminifu kutokana na kushindwa kuelewa makusudi ya kifaa hicho cha mawasiliano. Wengi wamechukulia simu ya mkononi ni kichaka cha maovu.

Somo la simu nilishawahi kuelezea, nilisema mapenzi ya kweli ya mtu hayakai kwenye simu, bali moyoni. Kuna watu huwashutumu wapenzi wao kwa kuchelewa kupokea simu.

Mawazo yao huwa ni kwamba, kama mpenzi hapokei simu, muda huo huwa anamsaliti, kumbe simu imo ndani yeye yupo nje.

Simu ya mkononi imekuwa ikiwaingiza watoto wa kike kwenye uhusiano bila kujijua. Nimekuwa nikiwafuatilia wasichana wote wenye simu hasa zenye mitandao.

Wengi wameingia katika mkumbo wa kuwa na simu zenye mtandao ili waweze kuchati kwenye Facebook, suala ambalo nimegundua linakula muda mwingi wa wasichana, kiasi cha kuwatoa kwenye utaratibu wao wa kawaida.

Hasara yake ipi?
Simu ya mkononi inawafanya baadhi ya kinadada kuwa na wapenzi wengi, pia hata kuweza kufika eneo la kukutana kwa wakati kwa vile mawasiliano yapo.

Kingine kibaya ni kwamba, kwa wanafunzi, uwezo wa darasani hupungua kutokana na muda mwingi kufikiria kuchati kwenye BBM, Twitter na Facebook, pia kuwa na mawiliano na wapenzi huwatoa wengi kwenye masomo.

Vitu hivi vimekuwa vikimwendesha msichana na kuamini hayo ndiyo maisha na kusahau kila kitu kina wakati wake. Hakuna mwanadamu aliyekamilika asiyetaka kuwa na mpenzi kwa vile kilele cha mhemko ni mshindo.

Lakini kwa wanafunzi, kwa vile bado wana wajibu wa kusoma ili kufikia malengo yao, mapenzi kwao ni vema yafanyike muda ukifika.

Simu imekuwa kichocheo cha watoto wa kike kuwa na wapenzi wengi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushindana na hoja za upande wa pili za mwanaume. Wengi wamekuwa wakipotea kwa kukubali kufanya ngono ili wapate simu kwa vile wao ni fasheni wala si kitendea kazi.

Tangu zilipokuja simu zenye uwezo wa kuwa na mitandao ya ziada, wasichana wengi wamepoteza uwezo wa kuwaza masomo, badala yake wanakesha kwenye mtandao wakichati.

Nina imani wasichana wengi wanaporomoka kiuwezo na kuwaacha wavulana wakiendelea kuwa wababe, kwa sababu tu ya suala hilo la simu.

Shule zenye maadili, hasa za bweni, ndizo zimekuwa zikizuia simu kwa wanafunzi lakini shule nyingi zimekuwa hazitilii mkazo suala hilo. Hata wazazi tumekuwa watu wa kuangalia tu mpaka mpaka mambo yaharibike.

Muda bado, hebu kaeni chini na watoto wenu na kuwaeleza, muda haurudi mara mbili, kama mzazi ulifanya makosa kwenye elimu basi mtoto asiyarudie.

Pia, nawe mtoto wa kike ambaye upo kwenye hatari kubwa, jitambue upo kwenye hali gani, jiepushe na starehe, heshimu malengo yako, kuwa na wivu wa kimaendeleo kwa kuamini kila kitu kina wakati wake. Kuwa na wivu wa maendeleo, timiza ndoto yako.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake