Friday, September 14, 2012

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA RASMI YA RAIS KIKWETE NCHINI KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mwenyeji wao Rais Mwai E. Kibaki baada ya kuwasili nchini Kenya, Jumanne, 11 Septemba , 2012, kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya. 
Juu na chini ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiajiandaa kwa Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili majirani na wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wake wa Chuo Kikuu cha Kenyatta baada ya kufungua Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akitembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja ya wakuu na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, na baadaye kupiga picha ya pamoja na ujumbe wake, wanachuo na viongzozi wa chuo hicho. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. (Nyuma yake ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya. 
Juu na chini ni Baadhi ya mawaziri na maofisa waliondamana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Kenya 
Juu na chini ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipanda miti wakati walipozuru mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke utokao chini ya ardhi wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini Kenya. 
PICHA NA IKULU 
Kwa picha zaidi bofya read more


 

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake