Thursday, September 13, 2012

MTANZANIA RAJABU MAOJA AJIFUA KUMCHAPA MNAMIBIA!

Rajabu Maoja


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mtanzania Rajabu Maoja anajifua ili kumpa kipigo cha aina yake bondia wa Namibia Gottlieb Ndokosho katika mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika unaotambulika na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF). Mpambano huo uliopewa jina na “Vita ya Jangwa la Kalahari” utafanyika katika jiji la Windhoek, nchini Namibia tarehe 29 mwezi huu.

 Mtanzania Rajabu Maoja ni mmoja kati ya mabondia waliojizolea sifa kemkem katika mchezo wa ngumi za kulipwa akiwa na makao yake katika jiji la Tanga.

 Maoja amepigana mapambanoi 32 wakato Ngoboko ameshaingia ulingoni mara 14 akishinda mapambano yote.

 Wawili hawa watakutana katika ukumbi wa SKW Hall, Olympia ulioko kusini mashariki mwa jiji la Windhoek, nchini Namibia, ukumbi huu ndio mabandia wengi wa Namibia wanapokutana na mabondia wengi kutoka nje kila mara.

 Mpambano wa Maoja na Ndokosho unaratibiwa na Kinda Promotions chini ya promota mahiri nchini Namibia bwana Simon Nangolo anayeishi katika jiji la Windhoek!

 Bodi ya ngumi na mieleka ya Namibia itasimamia mpambano huo wakati Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Urarabuni na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mpambano huo!


 Katika mapambani ya utangulizi bondia Cecilia Pitiseni kutoka nchi ya Zimmabwe atakungutana na bondia wa Namibia.

 Mapambano haya yanayotambuliwa na IBF yako katika mpango kabambe wa programu ya “Utalii wa Michezo” ambao IBF/USBA imeridhi kuufadhili na kuuendesha katika bara la Afrika. Tanzania na Ghana ni nchi za majaribio!

 Programu hii itawapa mabondia wengi wa Kitanzania nafasi kadhaa wa kadha za kugombea mikanda ya IBF sehemu mbalimbali duniani na kuitangaza ya Tanzania!

 Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya kati, Ghuba ya Urarabu na Uajemi anawahimiza watanzania watumie fursa hii kuzitangaza biashara zao kupitia programu hii!

 Anazihimiza pia taasisi za kibiashara, watu binafsi na mashirika yanayotoa huduma kwa jamii kuitumia programu hii ya IBF kujitangaza.

Imetumwa na:


Onesmo Ngowi

Rais,

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi

(IBF President for Africa, Middle East, Arabian Gulf and Persian Gulf)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake