Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa
katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madai ya kukaidi
na kupuuza amri ya serikali.
Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil
alionyesha mchezo huo kwa jina "The river and the mountain" katika
ukumbi wa Tilapia Cultural Center taraehe 17 Agosti na pia katika ukumbi
mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.
Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia
Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza
la Luzira hadi siku ya jumatatu ,Septemba 17 ambapo kesi yake
inatarajiwa kuendelea.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake