RAIS WA SOMALIA ANUSURIKA KIFO LEO
Rais
mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika jaribio la kumuua
mjini Mogadishu.Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao ya rais
huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa anajiandaa
kufanya mkutano na waandishi wa habari.Taarifa zinasema kuwa waziri wa
mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati
wa shambulizi. Hata hivyo wawili hao wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne
wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake