Kalala Jr akiongoza kulishambulia jukwaa ndani ya Joker's Live Pub uliopo Iloganzara Mwanza. wengine ni Bakari Mandela, Venna na Maga.
Wimbo mpya wa Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" uitwao Nyumbani ni Nyumbani" usiku wa jana ulikuwa ni moja kati ya vivutio vikubwa katika onyesho la Twanga Pepeta lililofanyika Jijini Mwanza katika ukumbi wa Joker's Live Pub uliopo Iloganzara.
Twanga Pepeta ilianza kwa kupiga nyimbo zake zilizoipatia umaarufu mkubwa kama Mtu Pesa, Safari 2005, Walimwengu kisha walianza kupiga nyimbo zao zilizokuwa katika albamu zao za hivi karibuni kama Mwana Dar es salaam, Nazi Haivunji jiwe, baadaye ndipo zilipopigwa nyimbo zao mpya za Shamba la Twanga na Nyumbani ni Nyumbani ambayo iliyoonekana kupokewa vizuri zaidi na mashabiki.
Mwinjuma Muumini "Kocha wa Dunia" akiutendea haki wimbo wa "Nyumbani ni nyumbani". Muumini alikuwa ni mmoja ya waimbaji walioshangiliwa sana wakati alipoimba kipande chake.
Mary Kimwana na Kiongozi wa Bendi Luizer Mbutu.
Jumanne Said akiimba mbele ya umati wa mashabiki wa Mwanza waliojitokeza kuishuhudia Twanga ndani ya Jiji la Mwanza.(Picha kwa hisani ya Twanga Pepeta Blog)
No comments:
Post a Comment