ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 12, 2012

Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z’bar


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini

Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.



Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Oktoba 10 mwaka huu.

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

“Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii,” umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.






 
CHANZO: NIPASHE

7 comments:

Anonymous said...

Are you serious??? I thought sisi wote ni watanzania ndani ya mikoa yote nchini wether ni bara au zanzibar basi na sisi wa bara tuwape wazanzibari wote wanaoishi bara vitambulisho sawa na watoka nje. IM TRULLY SHOCKED TO READ THIS ARTICLE JAMANI HII NAOMBA IWEKWE SAWA, MZUNGU ANASEMA TIT FOR TAT. NA BARA AMKENI WAPEMBA WOTE WALIOCHUKUA ARDHI YETU NA KUJIVUNIA BARA KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI NA WAO WAPENI VIBALI VYA WATOKA NJE KAMA WANAVYOTUPA SISI WA BARA HUKO ZANZIBAR.

Anonymous said...

INAONEKANA UNA MARADHI YA KUPAGAWA, HIVI UKIAMBIWA MKE KACHUKULIWA JANA INAONEKANA UTATOA TALAKA KESHO

Anonymous said...

Inasikitisha sana kuona kuwa ndani ya Tanzania watu wanabaguana kwa misingi ya kijinga tu. Hapa ndio maana mikasa ya maangamizi haitaisha unguja na Pemba. Mikosi haitakoma kwa mwendo huu.... Ubaguzi utawamaliza watanzania kani Ndugu KIKWETE hujalisikia hili? Ama halikusumbui kwani unakaribia kumaliza muda wako wa U-Rais! Wa salaam, Mtanzania wa Ughaibuni

Anonymous said...

HAKUNA HAJA YA KUWA NA MUUNGANO KAMA VITAMBULISHO VITATOLEWA.

Anonymous said...

HIVYO BASI MUUNGANO WA TANZANIA HAUNA MAANA.

Anonymous said...

HIVYO MUUNGANO WA TANZANIA UNAONEKANA KAMA HAUNA MAANA YOYOTE INAONEKANA
ZANZIBAR HAWATAKI MUUNGANO,DALILI ZA MVUA NI MAWINGU.NAFIKIRI BAADHI YA VIONGOZI WA ZANZIBAR WANA MAWAZO FINYU HAWATAZAMI MBALI.

Anonymous said...

MIMI KATIKA MTAZAMO WANGU NAONA MUUNGANO HAUNA MAANA TENA, BORA TUNGEUVUNJA INAKUWAJE WATANZANIA BARA WANAOKAA VISIWANI WANAPEWA VITAMBULISHO VYA UKAAZI AMBAPO WATANZANIA WA VISIWANI WANAOKAA BARA HATUWAPI VITAMBULISHO VYA UKAAZI?KWANZA KABISA IDADI YA WAZANZIBARI WANAOKAA BARA NI KUBWA KULIKO YA WABARA WANAOKAA VISIWANI.NAFIKIRI BAADHI YA VIONGOZI WACHACHE WENYE MAWAZO FINYU HUKO ZANZIBARI AMBAO HAWATAZAMI MBALI NDIO WALIOZUA SUALA HILI KWA MASLAHI YAO BINAFSI BILA KUJALI MASLAHI YA WANANCHI WENGI TANZANIA VISIWANI,MWISHO NAPENDA KUKUMBUSHA METHALI MOJA YA KISWAHILI KUWA DALILI ZA MVUA NI MAWINGU,NAONA MUUNGANO WA TANZANIA UNAANZA KUMEGUKA TARATIBU.