Walemavu watatu kutoka nchini Ufaransa waliopanda Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni, wamerejea salama.
Safari ya walemavu hao walioambatana na kundi la wataalam wa lugha ya alama, daktari na wasaidizi wengine, walianza safari ya kupanda mlima huo Septemba 10, na kushuka Septemba 16, mwaka huu.
Mmoja kati yao amepooza kiuno na miguu na alipanda mlima huo akiwa kwenye baiskeli maalum ya magurudumu matatu huku wengine wakiwa na matatizo ya kuona na kusikia.
Akizungumza kwenye lango la kuteremkia mlima huo la Mweka, Doninique Veran (51), alisema ametimiza ndoto yake aliyokuwa nayo kabla ya kupata ulemavu wakati akiwa na umri wa miaka 28.
Alisema ndoto hiyo ilibaki kwenye karatasi lakini baada ya kutoka kwenye mbio za baiskeli za watu wenye ulemavu, aliamua kutafuta wafadhili mbalimbali wa kumfadhili safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Alifafanua kuwa hiyo ilitokana na mtu mmoja kumpa moyo kuwa anaweza kupanda mlima huo.
Alisema safari yao haikuwa ngumu sana kutokana na jinsi waongoza watalii walivyofanya kazi kubwa ya kuwapa moyo na kuwajali hadi walipotimiza ndoto yao ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Naye mwongoza watalii aliyefanya kazi ya kuwaongoza, Abel Beimoja, alisema ilikuwa kazi ngumu sana hasa kwa mlemavu anayetumia baiskeli kwani alihitaji watu wanne wa kuisukuma muda wote.
"Napenda kuwatia moyo watu wenye ulemavu wa Tanzania, wasiangalie ulemavu wao bali jinsi gani watatimiza ndoto zao. Huyu mama alipata ulemavu akiwa na miaka 28, lakini bado ametimiza ndoto yake kwa kushiriki michezo mbalimbali na kupanda mlima akiwa na miaka 51,” alisema.
Naye Mhifadhi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), Steven Moshi, akizungumza wakati wa kuwapokea wageni hao na kuwapa zawadi mbalimbali za Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), alisema Kinapa inajivunia watu hao kupanda mlima huo kwa kuwa wameonyesha kuwa hata mlemavu anaweza kupanda na kufika kileleni kujionea vivutio vilivyopo.
Alisema ni changamoto kubwa kwa Watanzania kwani idadi ya Watanzania wanaopanda mlima huo inazidi kupungua huku wageni kutoka nje wakiwa wengi.
"Hali hii inayoonyesha kuwa Watanzania bado hawana mwamko wa kutosha wa utalii wa ndani," alisema.
Naye mpigapicha wa kundi hilo, Isabella Chemin, alisema ilikuwa kazi ngumu sana kwani baiskeli ilihitaji kubebwa na watu wanane hadi tisa na kusukumwa na watu wanne, jambo lililowafanya waongoza watalii kufanya kazi ya ziada.
Walemavu wengine walipanda mlima huo ni Ronain Soler (30) na Laurance Marandoni.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment