Bandari Dar Mabingwa Inter-Ports Games
• Yang’ara na kuibuka na vikombe vingi
Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa jumla katika michezo ya inter-ports games ambayo imefanyika jijini Mwanza hivi karibuni na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Mh. Baraka Konisaga. Michezo hiyo imefanyika jijini huko kwa muda wa
siku tano ambapo zaidi ya wanamichezo 400 wafanyakazi wa Bandari
walishiriki michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, pete, kikapu,
riadha, bao na kuvuta kamba.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine
kwa wanamichezo hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliwaasa wanabandari
kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujenga afya zao lakini kubwa
zaidi kutekeleza majukumu yao ya kila siiku kwa ufanisi. “Leo isiwe
mwisho wa kushiriki michezo endeleeni kushiriki ili kuoboresha afya zenu
lakini pia niwashauri kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na mkumbuke
kwamba mmepewa dhamana kubwa na taifa lenu hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa,” amesema Konisaga.
Katika
michezo hiyo Bandari ya Dar es Salaam iliibuka na vikombe vingi zaidi
ambapo katika mpira wa soka waliibuka washindi wa kwanza kwa
kujinyakulia alama nyingi huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Makao
Makuu.
Kwa upande wa mpira wa pete mshindi ni Bandari ya Dar es
Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Katika mchezo
wa kikapu nafasi ya kwanza ilikwenda Makao Makuu wakati Bandari Tanga
wakinyakua nafasi ya pili. Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kuvuta kamba
wanaume ilikwenda kwa Bandari ya Dar es
Salaam na nafasi ya pili
ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga.nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Bandari
ya Dar es Salaam na Bandari ya Tanga ilishika nafasi ya pili.
Kwa
upande wa riadha Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena kidedea huku
Bandari ya Tanga ikishika nafasi ya pili. Kwa upande wa wakimbiaji mita
mia moja kwa wanawake medali ya dhahabu ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka
Makao Makuu, medali ya fedha ilikwenda kwa mkimbiaji wa Bandari ya Tanga
na mshindi wa tatu alikuwa mkibiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam
aliyeibuka na medali ya shaba.
Kwa upande wa wakimbiaji wa mita
mia moja wanaume medali ya dhahabu ilichukuliwa na mkimbiaji wa Bandari
ya Dar es Salaam, fedha mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na shaba
ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na
Kyela). Kwa upande wa mita mia nne wanawake dhabau ilikwenda Bandari ya
Dar es Salaam, fedha ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam na shaba
ilikwenda kwa mkimbiaji wa Makao Makuu. Kwa upande wa mita mia nne
wanaume dhahabu ilikwenda Tanga, fedha ilikwenda Makao Makuu na shaba
ilinyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wa mchezo
mkongwe na wa jadi maarufu kama bao, Bandari ya Dar es Salaam iliibuka
tena na ushindi wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga.
Kwa upande wa wachezaji bora wa kila mchezo, mlinda mlango mahiri wa
timu ya Mtwara, Douglas Bahati aliibuka mshindi. Kwa upande wa mchezo wa
mpira wa pete, Matalena Mhagama ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa
aliibuka kidedea na nafasi ya kwanza. Kwa upande wa timu bora ya kuvuta
kamba
Makao Makuu waliibuka na ushindi huku Bandari ya Mtwara
ikiibuka na ushindi wa timu bora yakuvuta kamba wanaume. Mchezaji bora
wa riadha ni Lucy Kyoma kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Bandari
zilizoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Bandari Dar es Salaam,
Mtwara, Tanga, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu yenyewe. Michezo
hiyo hufanyika mara moja kila mwaka kwa kuwashirikisha wanabandari na
hufanyika mara moja kwa kila kituo.

No comments:
Post a Comment