ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 26, 2012

BARAZA LA EID EL HAJJ BWAWANI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
 Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi alipowasili katika
 Viwanja vya Salama Bwawani kuhutubia Baraza la EID El
 Hajj,lililofanyika leo .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
 Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea salamu ya heshma ya kikosi cha
 polisi FFU,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa
 mgeni rasmi katika Baraza la EID EL HAJJ Leo.
 Baadhi ya askari wa Kikosi cha Polisi cha FFU wakitoa
 salamu ya heshma ya Gwaride kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
 Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili katika
 viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa mgeni rasmi kulihutubia Baraza
 la EID EL HAJJ Leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
 Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar
 Mussa Ali Mussa,baada ya kupokea salamu ya Hesha ya gwaride la Kikosi
 cha Polisi FFU,leo alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani
 Hotel,akiwa mgeni rasmi kulihutubia Baraza la EID EL HAJJ Leo
 Mawaziri Wanawake wa Serikali ya Mapinduzi ya
 Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa,wakimsikiliza Rais wa
 Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
 Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu
 katika baraza la Eid El Hajj,huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini
 Zanzibar leo.
 Baadhi ya Maw\aziri wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa,wakimsikiliza Rais wa
 Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
 Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu
 katika baraza la Eid El Hajj,huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini
Zanzibar leo.
 Juu na chini ni Wananchi na waislamu wa Zanzibar ,wakike na
 wakiume wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
 Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi
 na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj,huko
 Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
 Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi na waislamu wa
 Zanzibar katika baraza la EID El Hajj,lililofanyika katika Ukumbi wa
 salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar Leo.
 Baadhi ya Wananchi na Waislamu wakijipatia vitafunio
baada ya kumalizika Baraza la Eid El Hajj, lililohutubiwa na Rais wa
 Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
 Shein,katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar Leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
 Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf
 Mzee,(kushoto) na Waziri wa Miundimbinu na Mawasiliano Rashid
 Suleiman,baada ya kulihutubia Taifa katika Baraza la Eid El Hajj Leo
 katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
 Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi na
 Kinamama baada ya kuwahutubia wananchi katika Baraza la Eid El Hajj
 Leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar

Salma Said, Zanzibar (Octoba 26-2012)

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametoa ametangaza vita dhidi ya watu wenye kuchagua hali ya amani na utulivu akisema serikali yake imefikia ukomo wa uvumilivu.

Kauli hiyo imetolewa jana katika baraza la Eid El Hajj katika ukumbi wa Salama kwenye Hoteli ya Bwawani muda mfupi baada ya kumaliza sala ya Eid iliyosaliwa kitaifa katika msikiti wa Muembeshauri Mjini Unguja.

Akionesha kukerwa na vitendo vya fujo na vurugu vinavyojirudia mara kwa mara katika visiwa vya Zanzibar, Rais alisema polisi pamoja na vyombo vya usalama vimejipanga kukabiliana na hali hiyo pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wanaochochea fujo hizo.

“Napenda kukuhakikisheieni nyote kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watakaotishia amani ya nchi yetu...jeshi letu la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara kudhibiti vitendo vya vurugu na fujo” alisema huku akipigiwa makofi katika hafla hiyo.

Alisema serikali yake itatumia sheria na taratibu zilizopo ili kuvishughulikia vitendo vya uvunjaji wa amani vitakavyofanywa au kuchochewa na kikundi chochote visiwani Zanzibar.

Kauli ya Dk Shein imefuatia vurugu za hivi karibuni zilizotokea baada ya kutoweka kwa kiongozi wa taasisi za kiislamu, Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye baadae aliibuka na kusema kwamba alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi.

Hata hivyo polisi walikanusha kuhusika na kadhia hiyo na Rais Dk Shein jana alirudia kusema kuwa Sheikh Farid hakutekwa na kuwataka vijana kutojishirikisha katika vitendo vya uvunjifu wa amani.

Tayari Sheikh Farid na wenzake saba wanashitakiwa katika mahakama za wilzaya na mkoa kwa makosa mbali mbali ya uchochezi na uvunjifu wa amani pamoja na kuharibu mali za serikali na watu binafsi. Kesi hiyo inatearajiwa kuendelea Novemba 7 mwaka huu.

Rais alisema ili kufikia malengo ya serikali pamoja na watu binafsi katika katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi suala la amani na utulivu linahitaji kupewa kipaumbele hasa wakati huu ambapo serikali inategemea sekta ya utalii.

Akizungumzia kuhusu muelekeo wa uchumi na hali za maisha ya watu, Dk Shein alisisitiza juu ya kufanya kazi kwa bidii na hasa akitoa wito kwa wakulima kujitayarisha kwa ajili ya msimu wa kilimo unaotarajia kuanza mwezi huu.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo pamoja na matrekta ya kulimia mapema kabla ya mvua kubwa hazijaanza.

Aidha Rais aliwataka wananchi kutunza mazingira ikiwemo suala la kuacha tabia ya kuchimba mchanga kiholela, kukata miti na kuharibu vianzio vya maji kwani kufanya hivyo ni kuharibu mazingira.

No comments: