Sikukuu ya Halloween ambayo asili yake imetokea kwa wapagani wa Ulaya magharibi ni siku waliokua wakisherehekea kwa kukumbuka watu waliokufa na kuomba mizimu ya babu zao kabla ya jina la Halloween zamani ilikua ikijulikana kama All Hallows' Eve na kunapo karne ya 16 sikukuu hii ikabadilishwa jina na kuitwa Halloween kwa Tanzania siku hii ni kama vile ndugu zetu wa Mjini kasoro bahari wanapokwenda kwenye milima ya kolelo kuomba mizimu ili kusaidia kuleta mvua na kadhalika. Nchini Marekani nyumba hupambwa na mifano ya watu waliokufa au watu wenyewe kuvaa vinyago au nguo zinazofanana kama watu waliofufuka makaburini wiki mbili au tatu kabla ya siku ya siku hii huonyeshwa sinema za kutisha na tarehe ya kusherekea siku hii ni October 31 kila mwaka pia ni siku utakayoona watoto wakipita kila nyumba kubisha hodi huku wakiwa wamevaa nguo za Halloween na wenye nyumba huwapa pipi
mfano wa mtu aliyefufuka akiwa nje ya nyumba
Matambara mfano wa sanda yamening'inizwa juu ya mti
Watu wanavaa vinyago
Watu wanajipamba na mavazi kama waliofufuka toka makaburini
No comments:
Post a Comment