Kibaka akipewa kipigo baada ya kubainika kutakaka kuwaibia majeruhi na marehemu wa ajali iliyotokea huko Mbalizi Mbeya. Hapa wananchi wenye hasira wakigawana kiungo kimoja hadi kingine cha kibaka huyo hadi kupoteza maisha.
Maisha ya kibaka huyo yaliishia hapa hata bila kufanikiwa mipango yake hiyo ya kuwaibia majeruhi wa ajali hiyo na wale waliopoteza maisha. Baada ya kutoa msaada jamaa akataka kujipatia riziki kwa kutumia upenyo huo. Ndipo alivyo bainika na wanachi nwenye hasira kali waka muangukia kwa kipigo hadi umauti ukamfikia.
|
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea mapema leo mchana katika ajali mbaya ya Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wakati wengine wakiendelea kuokoa majeruhi wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na kutaka kumchomolea fedha “ waswahili huita mshiko”.
Asalale kijana huyo ambaye hajafahamika jina mpaka mauti yanamkuta katika tukio hilo alikwidwa na mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi wa kuku.
Hebu nisiendee mbali sana kodoa jicho hapa
Kwa hisani ya blog ya malafyaleleo |
4 comments:
Hivi ni kifungu kipi cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kinachosema mwizi eneo la ajali anatakiwa kupigwa hadi kufa? Huu ni unyama jamani. Mbona mafisadi wanaoiba mabilioni ya shilingi na kulisababishia taifa hasara na umasikini uliokithiri hawapigwi namna hiyo? Hicho kipigo ni kinyume na haki za binadamu. Ni nani kati ya hao watesi hawajawi kuiba au kufanya kosa lolote na hakuna aliyewaadhibu?
HATA KAMA KAIBA ( which no body can prove 100%) hakustahili kuuliwa.. Mob justice is not something we should be promoting as society . Serikali inabidi kukemea na kuelimisha Jamai katika hili.
This is against human rights and should be STOPPED.
hivi mtu unaua mwizi hivi alafu unarudi nyumbani kwako unakula kinapita kabisaaa....khaa jamani, huu ni unyama, inasikitisha sana, hakuna anae unga mkono wizi lakini kuwaua ni jambo baya sana, sijui kwanini serikali haiingilii kati...kweli bongo hakuna sheria...
Post a Comment