Na Faida Muyomba, Geita
JESHI la Polisi mkoani Geita, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Nyambaya, Kata ya Katoma, wilayani Geita, Bw. Masanja Ilanga (45), kwa tuhuma za kumbaka mwanaye mwenye miaka minne.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paulo, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku nyumbani kwa mtuhumiwa.
Alisema mtuhumiwa alikuwa katika matembezi na baada ya kurudi nyumbani, alimbeba mtoto huyo na kwenda naye chumbani na kumfanyia kitendo hicho cha ubakaji.
“Awali huyu mtoto alikuwa nje na mama yake, baba mtu alimchukua na kwenda naye chumbani, baada ya muda mfupi mkewe alisikia mtoto akilia kwa uchungu.
“Baada ya kuingia ndani, alikuta mtoto akitokwa na damu sehemu za siri, hali hiyo ilimfanya mama huyu apige kelele za kuomba msaada kwa majirani ambao walifika mara moja,” alisema Kamanda Paulo.
Aliongeza kuwa, majirani walishangazwa na tukio hilo hivyo walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka Kituo cha Polisi ambapo mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
'”Tunafanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha tukio hili kama limetokana na tamaa ya ngono, imani za kishirikina au sababu zingine ambazo hazijafahamika
“Baada ya hapo mtuhumiwa tutamfikisha mahakamani wiki hii kujibu tuhuma zinazomkabili,” alisema.
Katika tukio jingine, jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu, wilayani hapa Bw. Saltari Andrew (27), kwa tuhuma ya kukutwa na noti bandia zenye thamani ya sh.100,000.
Kamanda Paulo, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 27 mwaka huu, saa 10 jioni eneo la Benki ya CRDB, iliyopo Kata ya Kalangalala, mjini Geita.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa na noti 20 za sh. 5,000 akiwa katika harakati za kuziweka benki na bado anaendelea kuhojiwa ili kubaini alikozipata, atafikishwa mahakamani upepelezi ukikamilika.
Majira
1 comment:
tamaa ya ngono ni mbaya,,,,huyo bwana aliyebaka na huyo mwenye noti bandia wote funga jela miaka mingi mno. Asanteni BBC SWAHILI kwa kutujuza haya
Post a Comment