ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 19, 2012

Misa na Mazishi ya Baba yake Sarah Tekle Tamanu


Ndugu, Jamaa na Marafiki wakibeba Jeneza lililobeba mwili wa Baba yake Sarah Marehemu Tekle Tamamu kuingia kanisani kwa ajili ya Misa kabla ya maziko yaliyofanyika Alhamisi Oct 18, 2012 Gate Of Heaven, Silver Spring, Maryland.
Sarah (wapili toka kushoto) akisindikizwa na ndugu yake Irene (wakwanza kushoto) na marafiki zake wa karibu Latifa (wapili toka kulia) na Tamia kuingia Kanisani kwenye Misa ya kumuaga mpendwa baba yake ilyofanyika Alhamisi Oct 18, 2012 S St NW, Washington, DC'
  
Kulia ni Mama Sarah na Sarah kushoto 
Ndugu, Jamaa na marafiki waliojitokeza kwenye misa.
Misa ikiendelea
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiendelea na misa
 wawili kushoto (viti vya mbele) wa pili toka kulia ni mdogo wa marehemu na kulia ni Mke wa marehemu ambae ndie mama yake Sarah.
Watanzania na WaEthiopia wakijumuika na kushirikiana pamoja na Ndugu, Jamaa na Marafiki katika kumsindikiza marehemu Tekle Tamanu kwenye safari yake ya mwisho.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakaribu wakiwa makaburi ya Gate Of Heaven kwenye mazishi ya baba yake Sarah.
Jeneza lililobeba mwili wa baba yake Sarah likiwa juu ya itakayokua nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya Gate Of Heaven yaliyopo Silver Spring, Maryland.
Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Sarah na familia wakiwa katika sala ya kabla ya mazishi ya baba yake Sarah aliyezikwa Alhamisi Oct 18, 2012 Silver Spring, Maryland.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiwa kwenye majonzi wakati mazishi yakiendelea.
Mke wa marehemu (kushoto) na Sarah wa pili toka kulia (walio kaa) wakifarijiwa wakati wa mazishi ya mpendwa wao yakiendelea.

Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye mazishi ya mpendwa wao marehemu Tekle Tamanu yaliyofanyika Alhamisi Oct 18, 2012 Gete of Heaven, Silver Spring, Maryland.
kutoka kushoto ni Sophia Mombasa, Abdul na Missy T wakiwa kwenye mazishi ya baba yake Sarah.
Sarah akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa baba yake aliyezikwa Alhamisi Oct 18, 2012 Silver Spring, Maryland.

Picha kwa hisani ya Swahili Villa

No comments: