ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 18, 2012

SHUHUDIA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA



Hakika si kila ajali itokeayo barabarani husikitisha bali zipo ambazo pindi zinapotokea watu hufurahi na kustaajabu vile ajali ilivyotokea. Hivi ndivyo ilivyolikumba gari hilo dogo Toyota Spacio T 629BRL iliyokuwa ikitokea maeneo ya Uwanja wa Ndege kuelekea mjini na kupinduliwa kama inavyoonekana katika picha katika barabara ya Nyerere karibu na kituo cha Tazara jijini Dar es Salaam jana alasiri.
Mashuhuda wa ajali hii wanapasha kuwa waliona kama mchezo wa sinema gari hii ilivyokuwa ikipinduka kiasi hata dereva wake kuto kutambua na kushtuka gari ipo chali. Mashuhuda hao wanapasha kuwa chanzo ni kupigwa pasi na lori la mizigo.
Wanadai kuwa baada ya kupigwa pasi gari hilo dogo lilinasa katika ngao ya lori hilo na taratibu wakati yanaenda katika foleni basi walishtukia gari ikigeuzwa ilikotokea na mara wakashangaa matairi yapo hewani.
Polisi usalama barabarani walifika na kuchukua maelezo ya ajali na kisha kuomba wenyenguvu walinyanyue gari hilo ili kuepusha msongamano barabarani.
Walijitokeza watu na kulinyanyua gari hilo ambalo liliharibika vibaya upande mmoja ambao ulipigwa pasi kisha kuruka sarakasi.
Dereva wa gari hilo (shati nyeupe) hakupata madhara zaidi ya nae kustaajabu kulicho tokea. 
Picha na Father Kidevu Blog

No comments: