ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 22, 2012

TAHADHARI KWA WANANCHI WA TANZANIA KUHUSIANA NA SMS YA MABOMU 30 KUTOKA MALAWI



Kuna
taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message 
za simu kwamba kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100
na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi 
kuwa waangalifu. 
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake 
haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.

Wananchi wanashauriwa kutotuma 
taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.

Assah Mwambene 
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.

No comments: