ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 24, 2012

YANGA 3 POLISI DODOMA 0

Haruna Niyonzxma akiambaa na mpira
David Luhende akivuta tela lake 
Haruna Niyonzima baada ya kutia krosi 
Mbuyu Twite akimdhibiti Nicholas Kabipe wa Polisi, huku Nahodha Nsajigwa Shadrack akiwa tayari kutoa msaada 
Jerry Tegete akiwania mpira na beki wa Polisi 
Penalti...Msuva akiwa ameangushewa kwenye eneo la hatari na beki wa Polisi kulia 
Barthez amedaka 
Kocha Ernie Brandts akimpongeza Kavumbangu baada ya mechi, kulia Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro 
Kwa picha zaidi bofya read more
Hatari kwenye lango la Polisi 
Msuva akienda chini baada ya kupigwa kwanja na beki wa Polisi (hayupo pichani) 
Msuva akishangilia bao lake 
Hatari kwenye lango lango la Yanga 
Kavumbangu anamuwajibisha beki wa Polisi 
Kavumbangu anafanya vitu 
Kiiza katika mishe mishe 
Kiiza anakwenda 
Hatari kwenye lango la Yanga 
Nahodha Nsajigwa anatia krosi 
Kazi kazi 
Kavumbangu anazuia mpira uliopigwa na mchezaji wa Polisi
Msuva alipofunga bao lake 
Kavumbangu akichomoka kushangilia baada ya kufunga 
Tegete akishangilia na Kavumbangu 
Kavumbangu akisababisha 

YANGA YAZIDI KUNG'ARA LIGI KUU, AZAM YABANWA NA RUVU CHAMAZI 
Msuva kulia akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza. Kushoto ni Jerry Tegete na David Luhende 

Na Mahmoud Zubeiry 

YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Ushindi huo, unaifanya Yanga itimize pointi 17, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kusimama katika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 18, baada ya sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 

Ruvu walipata bao lao kupitia kwa Seif Abdallah na Kipre Tcheche akaisawazishia Azam. 

Uwanja wa Taifa, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na washambuliaji Simon Msuva na Didier Kavumbangu. 

Msuva alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya tano kabla ya dakika moja baadaye, Mrundi Kavumbangu naye kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo. 

Yanga ingekwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0 kama mkwaju wa penalti wa Haruna Niyonzima usingegonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya mabeki wa Polisi kuondosha kwenye hatari. 

Refa Alex Mahagi kutoka Mwanza alitoa penalti hiyo, baada ya Msuva kuangushwa na beki John Bosco kwenye eneo la hatari wakati anakwenda kufunga. 

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi tena na kuendelea kulishambulia lango la Polisi, ingawa walipoteza nafasi nyingi na kutumia moja tu, dakika ya 58, mfungaji Hamisi Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete. 

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union iliifunga 1-0 African Lyon Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Morogoro. 

Matokeo ya leo yanaziweka karibu mno, Simba, Azam na Yanga pale juu, kiasi kwamba ushindani na uhondo wa ligi hiyo unaongezeka. 

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Nahodha), Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu na David Luhende/Nizar Khalfan. 

Polisi; Manji Kulwa/Kondo Salum, Nahodha Bakari, John Bosco, Noel Msakwa, Salmin Kissi, Hamisi Mamiwa, Bantu Admin/Paul John, Paschal Maige, Mokili Rambo (Nahodha), Malimi Busungu na Nicholas Kabipe/Keneth Masumbuko. 

Katika mchezo wa awali wa utangulizi, Yanga B imeifunga TMK United ya Ligi Daraja la Pili, mabao 6-1 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Polisi Morogoro. 

Mabao ya Yanga yamefungwa na Georgeb Banda matatu katika dakika za 61, 70 na 72, Hussein Moshi dakika ya 12 na Rehani Rehani dakika ya 19 na 27, wakati la kufutia machozi la TMK United, lilifungwa na Abdi Hashimu dakika ya 62. PICHA kwa hisani ya (Ben Zubeiry)

No comments: